Event:Wiki Loves Sports 2025 — Wikamusi
Mandhari
🏆 Wiki Loves Sports Editathon 2025 🏆
[hariri | hariri chanzo]Karibu kwenye Editathon ya kipekee ya michezo duniani kupitia miradi ya Wikimedia!
- 📅 Tarehe: Alhamisi, 20 Novemba 2025
- 🕔 Muda: Kuanzia saa 3:00 asubuhi – Saa kumi 10:00 kamili alasiri
- 📍 Ukumbi: UDSM New Library
ℹ Kuhusu Tukio
[hariri | hariri chanzo]WikiLove Sports ni kampeni ya kimataifa ya Wikimedia inayolenga kuhamasisha na kuongeza maarifa yanayohusu michezo, wanamichezo, historia ya michezo, na matukio ya kimichezo katika Wikipedia na miradi mingine ya Wikimedia. Wakati huu itahusu Wikamusi pekee.
Katika Editathon hii, washiriki watapata nafasi ya:
- Kuandika na kuhariri makala mpya kuhusu michezo mbalimbali.
- Kuboresha makala zilizopo kwa kuongeza taarifa sahihi na marejeo ya kuaminika.
- Kujifunza ujuzi wa kuhariri Wikipedia na Commons kwa msaada wa wakufunzi wenye uzoefu.
- Kushirikiana na wanajamii wenye mapenzi ya michezo na maarifa huria.
🎯 Malengo ya Editathon
[hariri | hariri chanzo]- Kuongeza idadi ya maingizo bora zinazohusu michezo kwenye Wikamusi.
- Kukuza ushirikiano kati ya jamii ya Wikimedia na wadau wa michezo.
- Kuhamasisha kizazi kipya cha wachangiaji wa Wikipedia na miradi mingine ya Wikimedia.
- Kuweka kumbukumbu endelevu za michezo ya kitaifa na kimataifa.
👥 Nani anaweza kushiriki?
[hariri | hariri chanzo]- Wanawikipedia wapya na wa muda mrefu.
- Wapenzi wa michezo na wanahabari.
- Wanafunzi, walimu, na jamii kwa ujumla.
- Hakuna sharti la kuwa mtaalamu – utapewa mafunzo na mwongozo wa hatua kwa hatua.
✅ Nini cha kuleta?
[hariri | hariri chanzo]- Kompyuta mpakato (laptop) au kifaa cha kuhariria.
- Shauku ya michezo na hamasa ya kushiriki kujenga maarifa ya kidigitali.
- Akaunti ya Wikipedia (unaweza kufungua bure kabla ya tukio).
📢 Kwa nini ushiriki?
[hariri | hariri chanzo]- Utakuwa sehemu ya kampeni ya kimataifa inayochangia maendeleo ya maarifa huria.
- Utajifunza ujuzi mpya wa kidigitali na uandishi.
- Utapanua mtandao wako wa kijamii na kitaaluma.
- Utapata fursa ya kuchangia urithi wa michezo kwa vizazi vijavyo.
🔔 Usikose! Hii ni nafasi ya kipekee ya kutumia kalamu yako ya kidigitali kuandika historia ya michezo na kuibadilisha kuwa rasilimali ya bure kwa kila mtu duniani.