Event:Tanzania Wikimedians Leaders Summit 2026 - Zanzibar

Karibu katika ukurasa unaobeba maudhui yaliyojadiliwa katika Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya za Wikimedia hapa nchini Tanzania.
Tanzania Wikimedians Leaders Summit 2026 - Zanzibar ni mkutano ulioandaliwa na Viongozi wa Jumuiya za Wikimedia nchini Tanzania kwa uratibu wa Wikimedia Community User Group Tanzania (kwa kushirikiana na Jumuiya za Wanawikimedia Tanzania), kwa ushirikiano na Wikimedia User Group Kenya, Wikimedia User Group Nigeria pamoja na Wikimedia Foundation.
Mkutano huu unalenga kuwaleta pamoja viongozi na wanaharakati wa harakati za Wikimedia kutoka Afrika Mashariki kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kujenga uwezo wa viongozi, na kupanga mikakati ya pamoja kukuza maarifa huru katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Muhtasari wa tukio
[hariri | hariri chanzo]- Tarehe: 26.03.2026 – 29.03.2026
- Eneo: Zanzibar Beach Resort - Tanzania
- Waandaaji: Wikimedia Community User Group Tanzania (kwa kushirikiana na Jumuiya za Wanawikimedia wa Tanzania)
- Washirika: Wikimedia Kenya, Wikimedia Nigeria, Wikimedia Foundation
- Wadhamini: Wikimedia Foundation
Washiriki
[hariri | hariri chanzo]Jumuiya za Wikimedia
[hariri | hariri chanzo]- Wikimedia Community Tanzania
- Jenga Wikipedia ya Kiswahili
- Wikimedians of Arusha
- Wikimedians of Kilimanjaro
- Wikimedians of Tabora
- Zanzibar Wikimedians
- Wikistudent Wikimedians
- Global WikiEducation Initiative
- Wikimedia Kenya User Group
- Wikimedia Nigeria
- Wikimedia Foundation
Hapa ni Orodha ya washiriki kutoka junuiya tajwa hapo juu
| No | Name |
|---|---|
| 1 | Willy Buloso |
| 2 | Eben |
| 3 | Anuary Rajabu |
| 4 | Shagari Said |
| 5 | Clement Masele |
| 6 | Eid John |
| 7 | Justine Msechu |
| 8 | Otto Nyongole |
| 9 | Ndaro Festo |
| 10 | Antoni Mtavangu |
| 11 | Mohamed Lupinga |
| 12 | Husseyn Issa |
| 13 | Maryam Saleh |
| 14 | Alex Method |
| 15 | Pellagia Njau |
| 16 | Mary Calist |
| 17 | Abubakari Frenk |
| 18 | Winnie Kabinti |
| 19 | Carol Mwaura |
| 20 | Ally Kiliwasha |
Lengo
[hariri | hariri chanzo]Kujadili njia mbalimbali za ushirikiano na kukuza uchangiaji wa maudhui ya Kitanzania na Afrika Mashariki kwenye miradi ya Wikimedia. Pia Mkutano unalenga kupanua njia za kushirikiana na wadau wengine.
Malengo mengine
[hariri | hariri chanzo]- Kuimarisha ushirikiano kati ya jumuiya za Wikimedia Afrika Mashariki na Nigeria.
- Kuwajengea uwezo viongozi katika kusimamia miradi ya Wikimedia.
- Kupanga mkakati wa kukuza maudhui ya Kiswahili na kushughulikia pengo la kijinsia kwenye miradi ya Wikimedia.
- Kushirikishana uzoefu na mbinu bora za uendelevu wa jumuiya.
Ratiba
[hariri | hariri chanzo]Siku ya 1: Mikutano ya uongozi na mawasilisho kutoka kwa washirika.
[hariri | hariri chanzo]Kuunda Mustakabali: Mafunzo kutoka Kikao cha Mkakati cha Wikimedia Tanzania 2026
Siku ya 1 – Uchambuzi wa hali ya sasa wa miradi ya Wikipedia nchini Tanzania “tuko wapi sasa?” Tathmini ya mazingira yetu ya ndani na nje, ikijumuisha nguvu, udhaifu, fursa na changamoto.
Tarehe: Ijumaa, tarehe 27 Machi 2026
Muda: Saa 3:00 asubuhi – Saa 10:00 jioni
Mahali: Zanzibar Beach Resort
Lengo: Kufanya uchambuzi wa SWOT wa miradi ya Wikimedia nchini Tanzania
Agenda
[hariri | hariri chanzo]| Muda uliopangwa | Shughuli | Wahusika |
| 9:00 - 9:15 | Usajili na Mapokezi ya Washiriki | Iddy John |
| 9:15 - 9:30 |
|
Antoni Mtavangu
& |
| 9:30 - 10:30 | Kikao cha 1 -
|
Antoni & MuddyB |
| 10:30 - 11:00 | Mapumziko mafupi (Chai) | |
| 11:00 - 12:00 | Kikao cha 2: Kushirikishana mitazamo kutoka kwa wanachama wa SSA RFC, pamoja na tathmini ya changamoto za sasa za Harakati za Wikimedia Tanzania kutoka kwa RFC | Pellagia Njau & Hussein Issa |
| 12:00 - 13:00 | Kikao cha 3: Mawasiliano ya athari (impact) yetu nje ya mfumo wa Wikimedia | Winnie & Carol |
| 13:00 - 14:00 | Mapumziko ya Chakula cha Mchana | |
| 14:00 - 15:00 | Kikao cha 4 : Msaada wa WMF kwa Wikimedia nchini Tanzania na matokeo yake | Willy Buloso |
| 15:00 - 16:00 | Kikao cha 5 : Kubaini changamoto na tafakari
|
Wote + Willy Buloso |
| 16:00 - 16:30 | Hitimisho na hatua zinazofuata | |
| 19.00 - 20.00 | Chakula cha Jioni | Washiriki Wote |
Siku ya 2: Vikao kazi (workshops) juu ya usimamizi wa miradi na mikakati ya ufadhili
[hariri | hariri chanzo]Kuunda Mustakabali: Mafunzo kutoka Kikao cha Mkakati cha Wikimedia Tanzania 2026
Siku ya 2 – Mkakati wa pamoja: kubainisha mpango wa kimkakati wa pamoja kwa miaka 3 ijayo, kushughulikia changamoto kuu katika kusaidia jamii na makundi yetu, na kufikiria upya namna ya kushirikiana.
Tarehe: Jumamosi, tarehe 28 Machi 2026
Muda: Saa 3:00 asubuhi – Saa 7:00 mchana
Mahali: Zanzibar Beach Resort
Lengo: Mpango wa kimkakati wa muda mrefu kwa miradi ya Wikimedia nchini Tanzania
Agenda
[hariri | hariri chanzo]| Muda uliopangwa | Shughuli | Wahusika |
| 9:00 - 9:15 |
Mchezo/ Burudani |
Hussein & Iddy |
| 9:15- 9:20 | Muhtasari wa siku | Eben |
| 9:20-10:20 | Kujifunza kutoka Nigeria na Kenya | Olaniyani Olushola(nyongeza kutoka Kenya) |
| 10:20-10:40 | Mapumziko /Chai | Wote |
| 10:40 - 12:10 | Kikao cha 2 – Mwelekeo wa mbele wa Harakati za Wikimedia nchini Tanzania
Thematic Groups - 1. Uchangishaji wa fedha (Fundraising) & Uendelevu (Sustainability), 2. Ushirikiano & Ukuaji, 3. Uongozi, 4. Mkakati (Msaada, Athari na Mkakati) |
Willy (muhtasari na kuweka mwelekeo wa majadiliano)
Hussein, Justine, Eben,Antoni |
| 12:10 - 1:10 | Kikao cha 3 – Uwasilishaji wa matokeo ya Kikao cha 2 | Washiriki wote, viongozi wa makundi wakiwasilisha hoja kuu kutoka makundi yao |
| 1:10-1:40 | Hotuba ya kufunga na hatua zinazofuata | Willy |
| 1:40 - 14:00 | Picha ya pamoja | Wote |
| 14:00 - 14.30 | Chakula cha mchana | Wote |
| 16:00 - 19.00 | Matembezi | Wote |
- Siku ya 3: Mpango wa pamoja na tathmini ya mkutano.
Jinsi ya Kujiunga
[hariri | hariri chanzo]Ili kujiunga na tukio hili, tafadhali jisajili kupitia kiungo cha usajili. Hakikisha una akaunti ya Wikimedia.

Kiungo cha Jumuiya Shiriki
[hariri | hariri chanzo]- Wikimedia Community User Group Tanzania: wikitzagroup@gmail.com
Matukio katika picha
[hariri | hariri chanzo]Itakujia hivi punde....