Event:Shindano la Kuandika Wikipedia na Wikamusi – WikiGap JWK 2026
TANGAZO LA EVENT: Mashindano ya Kuandika Wikipedia na Wikamusi – WikiGap JWK 2026
Katika kuadhimisha kampeni ya WikiGap 2026, Jenga Wikipedia ya Kiswahili (Affiliate) inapenda kuwatanagazia kuanza kwa shindano la kuandika makala za Wikipedia na Ingizo za Wikamusi (WikiGap JWK 2026), yanayolenga kuongeza na kuboresha maudhui yanayohusu wanawake katika miradi ya Wikimedia kwa lugha ya Kiswahili.
Shindano hili ni sehemu ya juhudi za kupunguza pengo la kijinsia katika maarifa huria, kwa kuhamasisha uandishi wa makala na maneno yanayoangazia mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za kijamii na kitaaluma.
Maudhui ya shindano
[hariri | hariri chanzo]Washiriki wanakaribishwa kuandika au kuboresha:
Wikipedia
Makala zinazowahusu wanawake katika nyanja zifuatazo:
Siasa
Sayansi
Muziki na sanaa
Harakati za kijamii
Malezi
Afya
Uchaguzi
[hariri | hariri chanzo]Uchaguzi wa mada ni wa hiari, mradi tu makala inamhusu mwanamke na inazingatia sera na miongozo ya Wikipedia.
📂 Makala zote lazima ziwekwe katika: Jamii:WikiGap JWK 2026
Wikamusi
[hariri | hariri chanzo]Washiriki wanaweza pia kuandika au kuboresha ingizo la maneno katika Wikamusi kulingana na miongozo ya mradi huo.
Muda wa shindano
[hariri | hariri chanzo]📅 Kuanzia: Januari 2026 📅 Mwisho: 15 Machi 2026
Tathmini na Alama
Kila kazi itapimwa kwa mfumo wa alama 0–10
Vigezo tofauti vitatumika kwa Wikipedia na Wikamusi
Kazi zitakazokiuka sera au kufutwa hazitatathminiwa
Zawadi kwa washindi
[hariri | hariri chanzo]🏆 Mshindi wa Kwanza: Vocha ya TZS 150,000 🥈
Mshindi wa Pili: Vocha ya TZS 130,000
Mshindi wa Tatu: Vocha ya TZS 100,000
Nafasi ya Nne: Vocha ya TZS 80,000
Nafasi ya Tano: Vocha ya TZS 60,000
Tukio la uzinduzi
[hariri | hariri chanzo]📍 Ukumbi: (utatangazwa)
📅 Tarehe: (itatangazwa)
Tukio hili litaleta pamoja wahariri wapya na waliopo kwa ajili ya utambulisho wa mashindano, mafunzo mafupi, na maswali na majibu.
Nani Anaweza Kushiriki
Wahariri wapya na waliopo wa Wikipedia na Wikamusi
Yeyote mwenye nia ya kuchangia maarifa huria kwa lugha ya Kiswahili.
Dashibodi
[hariri | hariri chanzo]Jiunge hapa kwa kuweka rekodi: https://outreachdashboard.wmflabs.org/courses/Jenga_Wikipedia_ya_Kiswahili/WikiGap_Campaign_for_2026?enroll=tgehckuz