Nenda kwa yaliyomo

Eva Herzigová

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eva Herzigová

Eva Herzigová (matamshi ya Kicheki: [ˈɛva ˈɦɛrzɪɡovaː]; alizaliwa 10 Machi 1973) ni mwanamitindo, mwigizaji na mwandishi wa habari za mitindo kutoka Czechia. Mwaka 1994, alikua sura ya kampeni ya Wonderbra iliyokuwa na kauli mbiu “Hello Boys”. Urefu wake wa mita 1.80 (futi 5 na inchi 11) pamoja na mwonekano wake wa kifahari ulimfanya kuwa mwanamitindo aliyekuwa akitafutwa sana kwa maonyesho ya mitindo na kampeni za chapa mbalimbali maarufu.

Katika kipindi chote cha kazi yake, Herzigová amefanya kazi na wabunifu na nyumba maarufu za mitindo, zikiwemo Dolce & Gabbana, Chanel, Versace na Louis Vuitton, na ameonekana kwenye majalada ya majarida mengi mashuhuri ya mitindo kama Vogue, Elle, Harper's Bazaar, Marie Claire, Cosmopolitan, Glamour na mengine mengi. [1][2]

  1. ↑ https://www.imdb.com/name/nm0381283/
  2. ↑ https://www.fashionmodeldirectory.com/models/eva_herzigova/
Makala hii kuhusu mwanamitindo fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eva Herzigová kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.