Eustasi wa Luxeuil

Eustasi wa Luxeuil (560 hivi – 629 hivi) alikuwa abati wa pili wa Luxeuil kuanzia mwaka 611, akimrithi mwalimu wake Kolumbani, baada ya kuwa mkuu wa chuo cha monasteri.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Eustasi alizaliwa huko Burgundy (leo nchini Ufaransa) akatawa huko Luxeuil.
Kolumbani, mwanzilishi wa abasia hiyo, alipofukuzwa na mfalme wa Burgundy kwa sababu ya kukemea maadili yake, alimpendekeza Eustasi achaguliwe kushika nafasi yake, akahamia Bobbio, Italia.[2][3]
Eustasi alikuwa mtu mnyenyekevu, wa sala na mfungo wa kudumu.
Chini yake, monasteri ilizidi kusifiwa kwa elimu na utakatifu wa wamonaki wake 600 [4]. Pamoja na baadhi yao alijitosa kuhubiri maeneo yasiyoinjilishwa bado, hasa katika Galia ya kaskazini-mashariki, lakini pia Bavaria. Wengine wakawa maaskofu na watakatifu.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Stohlmann, Jürgen (2003). "Eustasius von Luxeuil". Lexikon der Heiligen und der Heiligenverehrung. Juz. la 1. Freiburg im Breisgau: Herder. ISBN 3-451-28191-0.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint of the Day, March 29: Eustace of Luxeuil Ilihifadhiwa 24 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine. at SaintPatrickDC.org
- (Kijerumani) Biografie der Diözesanbibliothek Münster
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |