Eugène Moke Motsüri
Mandhari
Eugène Moke Motsüri (25 Machi 1916 – 6 Aprili 2015) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alikuwa mmoja wa maaskofu waliokuwa hai kwa muda mrefu na askofu mzee zaidi barani Afrika hadi kifo chake tarehe 6 Aprili 2015.
Motsüri alizaliwa katika Mongobele, wakati huo sehemu ya Kongo ya Kibelgiji, na alipadrishwa tarehe 9 Juni 1946. Aliteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Kinshasa na askofu wa jimbojina la Lestona tarehe 1 Septemba 1970. Aliendelea kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Kinshasa hadi alipostaafu tarehe 11 Mei 1991.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |