Eubulo wa Kaisarea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eubulo wa Kaisarea (alifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 308) alikuwa Mkristo wa Batanea (leo nchini Syria) ambaye wakati wa dhuluma ya kaisari Dioklesyano alikwenda Kaisarea kuhudumia waliodhulumiwa[1] akateswa mwenyewe pia kwa sababu ya imani yake[2] akatupwa kwa simba kuliwa siku mbili baada ya mwenzake Adriano. Hatimaye alimalizwa kwa upanga.[3][4].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadimishwa tarehe 7 Machi[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.