Etweda Cooper
Etweda Ambavi Gbenyon Cooper, anayejulikana kwa jina la Sugars, ni mwanasiasa na mwanaharakati wa amani kutoka Liberia. Ameelezewa kama “mama mkubwa (doyenne)” na “mama wa harakati” wa harakati za wanawake nchini Liberia. Mwaka 2010, alichaguliwa kuwa meya wa mji wa Edina, Liberia. Baadaye alihudumu kama msimamizi mkuu wa Kaunti ya Grand Bassa kuanzia mwaka 2012 hadi 2015.[1][2][3]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Etweda Cooper alizaliwa mjini Edina, katika familia ya tabaka la juu iliyotokana na watumwa waliokuwa wameachiliwa huru, waliotoka Marekani na kuhamia Liberia katika karne ya 19. Alikulia akizungumza Kibassa na Kiingereza cha Liberia. Cooper anajulikana kote nchini kwa jina lake la utani, Sugars. Aliondoka Liberia akiwa kijana na kwenda kusoma chuo kikuu mjini Bern, Uswisi.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Feminism's Vital Role in Rebuilding Liberia". The Root (kwa American English). 2010-12-24. Iliwekwa mnamo 2021-01-22.
- ↑ Gbowee, Leymah (2011). Mighty Be Our Powers: How Sisterhood, Prayer, and Sex Changed a Nation at War. Mithers, Carol Lynn. New York: PublicAffairs. ISBN 978-0-9842951-5-9. OCLC 751747258.
- ↑ Tripp, Aili Mari (2015). Women and Power in Postconflict Africa. Cambridge University Press. ISBN 9781316432495.
- ↑ Robbins, Ed (2011-02-08). "Liberia Beyond Monrovia: A Small-Town Mayor's Big Visions for the Future". International Reporting Project.
| Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Etweda Cooper Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |