Nenda kwa yaliyomo

Etim Inyang

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Etim Okon Inyang (25 Desemba 1930 - 26 Septemba 2016) alikuwa Afisa wa Polisi wa Nigeria na aliyewahi kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi. Alihudumu kuanzia mwaka 1983 akichukua nafasi ya Sunday Adewusi, na alifuatwa na Muhammadu Gambo Jimeta mwaka 1986. [1] [2] Alifariki akiwa na umri wa miaka 84 jijini Lagos Nigeria.

Inyang alizaliwa Enwang Mbo, Akwa ibom, akiwa mtoto wa Okon Inyang, mtawala wa kimila wa Enwang. Alipata elimu yake katika shule ya kikatoliki ya Roma, Uko-Akpan(1936-1937) shule ya Wametodisti(1939-1940) na shule ya Oyubia, Oron(1941-1945). Kabla ya kujiunga na jeshi la polisi. inyang alikuwa mwalimu kati ya miaka ya 1946 na 1949.

  1. "Abba Police go Police come". dailyindependentnig.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "List of Inspector General of Police in Nigeria". the-nigeria.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Julai 2018. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)