Esther Murugi Mathenge
Esther Murugi Mathenge ni mwanasiasa wa Kenya. Awali alikuwa Mjumbe wa Bunge la Kitaifa la Kenya akiwakilisha Jimbo la Nyeri.
Kazi ya Kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Esther Murugi Mathenge alikuwa Waziri wa Programu Maalumu katika serikali ya muungano wa Kibaki na Raila. Alianza kuwania nafasi ya kisiasa katika uchaguzi wa Kenya wa mwaka 2002.Pia alichaguliwa chini ya chama cha National Unity katika uchaguzi wa bunge la Kenya wa mwaka 2007.
Murugi aliendelea kushikilia wadhifa huo katika uchaguzi wa mwaka 2013 akiwa na chama cha The National Alliance , katika kipindi cha Jubilee ya Uhuru Kenyatta na William Ruto, na kuwa mtu wa kwanza kihistoria kushikilia kiti cha bunge cha Nyeri mara mbili mfululizo. Hata hivyo, alipoteza kiti hicho katika uchaguzi wa mwaka 2017.[1]
Anakumbukwa pia kama mwanamke wa pili kushinda uchaguzi katika Kaunti ya Nyeri baada ya Profesa Wangari Maathai kushinda kiti cha bunge cha Tetu mwaka 2002.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Esther Murugi Mathenge kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-16. Iliwekwa mnamo 2026-01-31.