Nenda kwa yaliyomo

Esi Awuah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Esi Awuah ni Balozi wa kutokea nchini Ghana kwa nchi ya Uswisi, msomi na makamu mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Nishati na Maliasili huko Sunyani, Ghana. [1] [2] [3]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Awuah ni mtoto wa kwanza wa Emmanuel Broni Asare na Margaret Annan. Baba yake anatokea Akim Oda kwenye Mkoa wa Mashariki wa Ghana, na alishika nafasi ya Naibu Mhifadhi Mkuu wa Misitu kwenye maeneo ya Ashanti na Brong-Ahafo . Mama yake, Margaret Annan, ni msaidizi muuguzi mstaafu anatokea kijiji cha Gomoa Dago nchini Ghana. Awuah alipokea elimu yake ya kawaida ndani ya Akim Oda mnamo 1973 na kukamilisha elimu yake ya juu kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Aburi mnamo 1975. Alipata elimu ya Shahada ya Sayansi kwenye Sayansi ya Biolojia kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah (KNUST), Shahada ya Uzamili kwenye Sayansi ya Mazingira katika SUNY ESF Syracuse nchi ya Marekani na Shahada ya Uzamivu kwenye Matibabu ya Maji Taka katika Chuo Kikuu cha Wageningen /UNESCO-IHE Delft Uholanzi.

Hapo baadae alipohitimisha huduma yake ya kitaifa kwenye Taasisi ya Utafiti wa Bidhaa za Misitu huko Kumasi (sasa Taasisi ya Utafiti wa Misitu ya Ghana ). Awuah alipata nafasi ya kazi kama msaidizi wa utafiti kwenye Idara ya Uhandisi wa Kiraia. Mwaka 1981, alipata udhamini wa Shirika la Afya Duniani ili kusoma sayansi ya mazingira nchi ya Marekani kwenye Chuo Kikuu cha Jimbo la New York cha Sayansi ya Mazingira na Misitu huko eneo la Syracuse, New York . Mwaka 1998, alipewa ufadhili kutoka serikalini ya Uholanzi ili kufuatilia Shahada ya Uzamivu katika matibabu ya maji machafu katika Taasisi ya Uhandisi wa Miundombinu, Maji, na Mazingira (sasa UNESCO-IHE ) huko Delft nchini Uholanzi.

Awuah alianza kazi yake ya kitaaluma kwenye KNUST mwaka 1986 kwenye Idara ya Uhandisi wa Ujenzi. Alishika nafasi ya mhadhiri mkuu mwaka wa 1996, profesa msaidizi mwaka 2002, na akaomba uprofesa kamili mwaka 2008 na kumaliza mwaka 2014.

Awuah amefundisha kozi kwenye KNUST, Chuo Kikuu cha Cape Coast, na Chuo Kikuu cha Elimu, Winneba, kwa sekta zote mbili za shahada ya kwanza na ya uzamili. Pamoja na hayo ameandaa mitaala juu ya taaluma kadhaa zinazotumika kuanzisha programu za kitaaluma nchini Ghana na Liberia. [4]

Akiwa mtafiti mwenye malengo maalum kwenye usambazaji wa maji, usafi wa maeneo, matibabu ya maji taka, usafi, na tathmini ya hatari ya mazingira, Awuah aliongoza miradi kadhaa ya ufafanuajii wa ubora wa maji ili kuongeza uelewa kuhusu uchafuzi wa mazingira kwenye vijito vya mijini na uchafuzi wa maji ya ardhini kutoka kwa mifumo ya usafi wa mazingira ya ndani. Maendeleo yake ya utafiti ni ujumuishaji na mifumo ya kupima uzito kwa ajili ya tathmini ya athari za maendeleo ya maji nchini Ghana na kuondolewa kwa arseniki kutolewa kwa maji ya ardhini kwa kutumia vifaa vya ndani. Maeneo mengine yanayoangaziwa ni jumla na mifumo mikubwa ya kutoa vimelea kwenye mabwawa ya utulivu wa taka, jukumu la arseniki kwenye vidonda vya Buruli jumla na desturi za mazingira na sababu za hatari zinazohusiana na ugonjwa huo, sababu za hatari zinazohusiana na matumizi ya maji machafu kwenye kilimo, nafasi ya arseniki na athari za kiafya zinazohusianishwa na uzalishaji wa mkaa na usafi wa muuzaji wa chakula.

Awuah ana machapisho zaidi ya 100 yanayozunguka kwenye majarida yaliyorejelewa, karatasi za mikutano, ripoti za maeneo, na sura za vitabu. [4] Amekua mwangalizi wa zaidi ya wanafunzi 200 wa shahada ya kwanza na zaidi ya wanafunzi 50 wa shahada ya kwanza na kusimamia ushirikiano kadhaa wa utafiti wa kimataifa kwenye utoaji wa maji, afya ya mazingira, na usafi wa mazingira. Miongoni mwao ni mradi wa SWITCH unaoungwa mkono kiuchumi na EU juu ya usimamizi wa maji mijini na mradi wa CapWa juu ya ukusanyaji wa mvuke wa maji ili kuhifadhi maji na nishati kwenye viwanda, mradi wa African SNOWS kuhusu ujenzi wa uwezo wa utafiti kwa lengo la usambazaji wa maji, afya ya mazingira, na usafi wa mazingira, na mradi wa usafi wa mazingira wa SMART ili kuendeleza teknolojia za vyoo maalumu kwa maskini wa mijini. Miradi hii imezalisha mamilioni ya dola kwa shirika zinazohusika na zimemfanya Awuah kuwa mtaalamu wa kimataifa. [4]

Pamoja na kazi yake ya ualimu ya miaka 32, Awuah amehudumu kwenye nafasi kadhaa za uongozi kwenye KNUST. Alikuwa mkuu wa Idara ya Mazingira na Teknolojia katika Taasisi yake ya Sayansi na Teknolojia ya Afrika kutoka mwaka 2004 hadi mwaka 2006, mkuu wa idara ya Uhandisi wa Kiraia kuanzia 2006 hadi 2008, na mkuu wa Kitivo cha Uhandisi wa Kiraia na Jiosumaku kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010. Zaidi ya hayo, alishika nafasi katika Kamati ya Uteuzi na Utangazaji ya Chuo cha Uhandisi, Kamati ya Miundombinu ya Chuo, na Kamati ya Maktaba ya Chuo cha Uhandisi. Pamoja na hayo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu, na kama mshirika wa Bodi ya Kitivo cha Sayansi ya Jamii, ni mhadhiri anayehusika na Uhandisi wa Ubora wa Mazingira.

Yeye ni mjumbe kiongozi wa bodi ya utendaji, anayewakilisha eneo la Afrika, la Shirika la Wanawake katika Sayansi kwenye Nchi za uchumi wa chini, na anatumika kwenye bodi zingine kadhaa za ndani na ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Baraza la Ushirikiano la Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira Duniani, Wakfu wa Kimataifa wa Sayansi, SPLASH, Bodi ya EU ya Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira, Water Aid Ghana, na Zoom-lion Ghana Limited.

Mwishoni mwa mnamo 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, Awuah alibobea kwenye kushughulikia suala la VVU/UKIMWI. Pamoja na hayo aliongoza timu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cornell kuandaa warsha juu ya elimu ya usafi huko Bimbilla . Kikundi hicho pia kilinunua na kuweka pampu za maji kwenye jamii.

Miongoni mwa heshima zake za kitaaluma, Awuah alitunukiwa Tuzo ya UNESCO Mondialogo mwaka wa 2007 kwa utafiti bunifu juu ya uhandisi. [4] [5] Pamoja na hayo alitambuliwa mwaka wa 2008 na Wizara ya Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini nchini Ghana kipindi cha mwaka wa kimataifa wa usafi wa mazingira . Mwaka 2011, alipokea tuzo ya fedha kwa utafiti bora kwenye eneo la mazingira, maji, na usafi wa mazingira, wakati wa Kongamano la kwanza la Sayansi ya Kitaifa nchini Ghana.

Maisha ya kibinafsi

[hariri | hariri chanzo]

Awuah mshirika wa Kanisa la Methodisti la Mount Zion huko Kotei, Kumasi, ambapo yeye ni mpiga kinanda na mwimba kwaya. Ameolewa na RT Awuah, mtaalamu wa magonjwa ya mimea na Kiongozi wa zamani wa Chuo cha Kilimo kwenye Chuo Kikuu cha Elimu, Winneba (Kampasi ya Ashanti Mampong), pamoja na kua mkuu wa zamani wa Kitivo cha Kilimo huko KNUST. Wanandoa hao wana watoto wawili, Ato na Kobbina.

  1. "Prof Esi Awuah calls for a shift from grades-oriented curricula". 12 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Energy & Natural Resources University, blessing for Ghana-VC". GhanaWeb. 4 Mei 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Mei 2012. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Ghana inducts second female University Vice Chancellor". GhanaToGhana. 18 Novemba 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 1 2 3 4 "Mrs. Esi Awuah, Prof. (Senior Member)". University of Energy and Natural Resources. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Agosti 2014. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "UENR" defined multiple times with different content
  5. "Environmental Sanitation is a way of life". Levers in Heels. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Agosti 2014. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Vyungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]