Ndwindwi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Erythrocercidae)
Ndwindwi
Ndwindwi manjano (Erythrocercus holochlorus)
Ndwindwi manjano (Erythrocercus holochlorus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Erythrocercidae (Ndege walio na mnasaba na ndwindwi)
Jenasi: Erythrocercus
Hartlaub, 1857
Ngazi za chini

Spishi 3:

Ndwindwi au dwidwi ni ndege wadogo wa jenasi Erythrocercus, jenasi pekee ya familia Erythrocercidae. Ndwindwi wanafanana na chechele, lakini bila mkia mrefu sana, na kwa hivyo zamani waliainishwa katika familia Monarchidae. Jina la jenasi linatoka lugha ya Kiyunani: ερυθρος = nyekundu na κερκος = mkia. Mbili baina ya spishi tatu zina mkia mwekundu kwa kweli lakini ile ya tatu ina mkia njano. Ndwindwi wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na malaika. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]