Eric Maxim Choupo-Moting

Jean-Eric Maxim Choupo-Moting (alizaliwa 23 Machi 1989) ni mchezaji wa soka wa mwenye asili ya Kijerumani na Kamerun, anayecheza kama mshambuliaji katika klabu ya New York Red Bulls ya Major League Soccer (MLS). Alizaliwa nchini Ujerumani, lakini anaiwakilisha timu ya taifa ya Kamerun katika michuano ya kimataifa.[1]
Choupo-Moting alianza taaluma yake Hamburger SV, ambapo alicheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi ya Ujeruman Bundesliga mnamo Agosti 2007. Msimu wa 2009–10, alicheza kwa mkopo katika timu za 1. FC Nürnberg, kabla ya kujiunga na 1. FSV Mainz 05 mnamo Agosti 2011. Baada ya misimu mitatu ya mafanikio na Mainz, alihamia Schalke 04 mwaka 2014, ambako alicheza zaidi ya mechi 80 na kufunga mabao kadhaa muhimu.[2]
Mnamo Agosti 2017, alijiunga na Stoke City ya Premier League, kabla ya kuhamia Paris Saint-Germain (PSG) mnamo Agosti 2018, ambako alishinda mataji ya Ligue 1 na kufikia fainali ya UEFA Champions League mwaka 2020.
Baada ya kumaliza muda wake na PSG, Choupo-Moting alisaini mkataba na Bayern Munich mnamo Oktoba 2020, akishinda mataji kadhaa ya ndani na kimataifa, ikiwemo Bundesliga na Kombe la Dunia la Klabu ya FIFA.
Baada ya kumaliza mkataba wake na Bayern mwishoni mwa msimu wa 2023–24, alijiunga na New York Red Bulls mnamo Desemba 2024 kama mchezaji huru, akianza sura mpya ya taaluma yake katika soka la Marekani.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Choupo-Moting verzichtet auf Afrika-Cup". Kicker (kwa Kijerumani). 3 Januari 2017. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2017.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Choupo-Moting, Eric Maxim" (kwa Kijerumani). Kicker. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2014.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eric Maxim Choupo-Moting kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |