Eric Bach

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eric Bach ni mtaalamu wa kompyuta aliyetoa mchango kwenye nadharia ya mahesabu ya namba.

Alimaliza elimu yake ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Michigan, Ann Arbor, na alipata Ph.D yake kwenye sayansi ya kompyuta kutoka chuo cha Kalifornia, Berkeley, mwaka 1984 chini ya usimamizi wa Manuel Blum[1]. Kwa sasa ni profesa kwenye kitengo cha sayansi ya kompyuta Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Manuel Blum". www.cs.cmu.edu. Iliwekwa mnamo 2022-09-09. 
  2. https://pages.cs.wisc.edu/~bach/bach.html