Nenda kwa yaliyomo

Guinea ya Ikweta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Equatorial Guinea)
Jamhuri ya Gine ya Ikweta
República de Guinea Ecuatorial (Kihispania)
République de Guinée équatoriale (Kifaransa)
República da Guiné Equatorial (Kireno)
Kaulimbiu ya taifa:
Unidad, Paz, Justicia (Kihispania)
"Umoja, Amani, Haki"
Wimbo wa taifa:
Caminemos pisando las sendas de nuestra inmensa felicidad (Kihispania)
"Tutembee tukifuata njia za furaha yetu kubwa"
Mahali pa Guinea ya Ikweta
Mahali pa Guinea ya Ikweta
Ramani ya Guinea ya Ikweta
Ramani ya Guinea ya Ikweta
Mji mkuuMalabo
3°44′ N 8°46′ E
Mji mkubwa nchiniBata
01°51′ N 09°46′ E
Lugha rasmiKihispania
Kifaransa
Kireno
SerikaliUdikteta
 • RaisTeodoro Obiang
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 28 050[1]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 20231 737 695[1]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaPunguko USD bilioni 10.041[2]
 • Kwa kila mtuPunguko USD 6 502[2]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaPunguko USD bilioni 28.356[2]
 • Kwa kila mtuPunguko USD 18 362[2]
Maendeleo (2021)Ongezeko 0.596[3] - wastani
SarafuFaranga ya CFA
Majira ya saaUTC+1
Msimbo wa simu+240
Msimbo wa ISO 3166GQ
Jina la kikoa.gq

Gine ya Ikweta (pia: Ginekweta au Guinea ya Ikweta), kirasmi Jamhuri ya Gine ya Ikweta, ni nchi mojawapo ndogo ya Afrika iliyopo upande wa magharibi wa Afrika ya Kati.

Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon upande wa kusini na mashariki, na Ghuba ya Gine upande wa magharibi, ambapo visiwa vya São Tomé na Príncipe vinapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya Ikweta.

Jina la nchi linatokana na kuwa karibu na Ghuba ya Guinea na Ikweta.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Nchi ina sehemu mbili kuu. Eneo kubwa liko kwenye bara la Afrika katika kanda ya Rio Muni. Ndipo walipo wakazi wengi zaidi.

Sehemu iliyoendelea zaidi, pamoja na mji mkuu, iko kwenye kisiwa cha Bioko. Pamoja na visiwa vingine, hasa Annobon, hiyo kanda ya Visiwa ni sehemu ya pili ya nchi.

Bioko inavyoonekana kutoka Kamerun.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ilikuwa koloni la Hispania kwa jina la Guinea ya Kihispania likiwa na maeneo mawili ambayo yalijulikana kama Río Muni (bara na visiwa vidogo kadhaa), na kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Poo) ambako uko mji mkuu, Malabo (ambayo iliitwa awali Santa Isabela).

Mikoa ya Guinea ya Ikweta

Guinea ya Ikweta imegawiwa katika mikoa 8 iliyopo katika kanda mbili:

  1. Mkoa wa Annobón (mji mkuu wa mkoa: San Antonio de Palé)
  2. Mkoa wa Bioko Norte (Malabo)
  3. Mkoa wa Bioko Sur (Luba)
  4. Mkoa wa Centro Sur (Evinayong)
  5. Mkoa wa Kié-Ntem (Ebebiyín)
  6. mkoa wa Litoral (Bata)
  7. Mkoa wa Wele-Nzas (Mongomo)
  8. Mkoa wa Djibloho (Ciudad de la Paz)

Wananchi wengi (80%) ni wa kabila la Wafang, ambao ni wa Kibantu.

Ni nchi pekee ya Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndiyo lugha rasmi na ya taifa, hasa ukiacha Ceuta na Melilla (maeneo ya Hispania yaliyozungukwa na Moroko) na Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu (nchi isiyotambulika kimataifa). Pamoja nacho, Kifaransa na Kireno pia ni lugha rasmi.

Wananchi wengi wanafuata Ukristo katika Kanisa Katoliki (88%) na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti (5%). Wanaofuata dini asilia za Kiafrika na Baha'i ni 5%. Waislamu ni 2%.

Utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 "Equatorial Guinea". The World Factbook (kwa Kiingereza) (toleo la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 28 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (GQ)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 19 Oktoba 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Human Development Report 2021/2022" (PDF) (kwa Kiingereza). United Nations Development Programme. 8 Septemba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-10-09. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Uchambuzi na Maelekezo

[hariri | hariri chanzo]

Koo na Makabila

[hariri | hariri chanzo]
  • African Pygmies (Utamaduni na mziki wa watu wa Guinea ya ikwete / picha na ukoo.)


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guinea ya Ikweta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.