Epiklesi

Epiklesi (kutoka Kigiriki: ἐπίκλησις, epiklesis, "kuitia juu"[1]) katika teolojia ya Ukristo inamaanisha tendo la kumuita Roho Mtakatifu juu ya watu au vitu, hasa wakati wa liturujia. Kwa namna ya pekee kuhusu ekaristi (Misa au Liturujia ya Kimungu) anaitwa kugeuza mkate na divai altareni vigeuke kuwa Mwili na Damu ya Kristo[2].
Katika anafora epiklesi hiyo inaweza kuwepo kabla au baada ya simulizi la Karamu ya mwisho. Tofauti hiyo imesababisha suala la wakati ambapo mkate na divai vinageuzwa: ni wakati wa padri kutamka maneno ya Yesu kwa Mitume wake (baada ya epiklesi) au wakati wa epiklesi (baada ya maneno ya Yesu katika Karamu ya mwisho)? Kwa kawaida Wakristo wa Magharibi wanakubali zaidi jibu la kwanza[3], kumbe Wakristo wa Mashariki lile la pili[4][5].
Mapokeo ya Kanisa la Roma yana epiklesi ya pili baada ya simulizi hilo ambayo inamuita Roho Mtakatifu juu ya waumini ili, kwa kushiriki mkate mmoja wa ekaristi, awageuze kuwa mwili mmoja na roho moja katika Kristo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "ἐπίκλησις". Logeion.
- ↑ "Epiklesis". Catholic Encyclopedia. Iliwekwa mnamo 2007-02-18.
- ↑ Khoo, Lorna Lock-Nah (2005). Wesleyan Eucharistic Spirituality: Its Nature, Sources and Future (kwa English). ATF Press. ku. 94–95. ISBN 978-1-920691-31-8.
{{cite book}}: CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ Pomazansky, Protopresbyter Michael; Rose, Seraphim, tr. (1984), Orthodox Dogmatic Theology, Platina CA: Saint Herman of Alaska Brotherhood, uk. 279, LOC # 84-051294
{{citation}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Pontifical Council for Promoting Christian Unity (14 Novemba 2001). "Admission to the Eucharist in Situations of Pastoral Necessity". L'Osservatore Romano. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2022 – kutoka EWTN.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Brulé, Pierre; Lebreton, Sylvain (2007). "La Banque de données sur les épiclèses divines (BDDE) du Crescam : sa philosophie". Kernos. Revue internationale et pluridisciplinaire de religion grecque antique. 20 (20): 217–228. doi:10.4000/kernos.189. ISSN 0776-3824.
- Le Quellec, Jean-Loïc; Sergent, Bernard (2017). Dictionnaire critique de mythologie. CNRS. ISBN 978-2-271-11736-6.
Marejeo mengine
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Epiklesis (photo)
- ccwatershed.org
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Epiklesi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |