Enzo Dieci
Enzo Dieci (alizaliwa Sassuolo, 28 Januari 1934) ni askofu wa Kanisa Katoliki kutoka Italia, ambaye aliacha Roma mnamo Desemba 2009 na sasa anahudumu kilometa 35 kutoka Lima katika Kanisa la Sagrado Corazon de Jesus.
Alipewa daraja takatifu ya upadre tarehe 17 Machi 1962.
Mnamo Aprili 7, 1992, aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbojina la Maura na Askofu Msaidizi wa Roma. Dieci alipokea daraja hiyo tarehe 26 Aprili kutoka kwa Papa Yohane Paulo II, ambapo Kardinali Franciszek Macharski na Angelo Sodano walikuwa washirika wa utoaji daraja.
Kama askofu msaidizi wa Roma, alimsaidia Kardinali Makamu, Agostino Vallini, katika usimamizi wa kila siku wa jimbo, ambao unateuliwa kwake na Papa. Dieci pia anahudumu kama mjumbe wa Ushirikiano wa Misheni kati ya Makanisa.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |