Nenda kwa yaliyomo

Enrique Angelelli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Enrique Ángel Angelelli Carletti (17 Julai 1923 – 4 Agosti 1976) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Argentina ambaye aliuawa wakati wa udikteta kutokana na uhusiano wake na masuala ya kijamii. Juhudi za Angelelli kwa "Kanisa la Maskini" zilitoa mfano wa baadaye kwa Papa Fransisko.[1]

Mchakato wa kutangaza utakatifu wake ulianza mwaka 2015. Mnamo Juni 2018, Papa Fransisko alitangaza kwamba alifariki kama shahidi wa imani, na kumruhusu Angelelli na wenzake watatu (mapadri Carlos de Dios Murias na Gabriel Longueville, na mlei Wenceslao Pedernera) kutangazwa wafiadini.

Angelelli na wenzake walitangazwa wenye heri katika Hifadhi ya Mji wa La Rioja, La Rioja, tarehe 27 Aprili 2019.[2]

  1. "Beatification of four modern martyrs to the faith in Argentina - Vatican News". 27 Aprili 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Meet the four countrymen of Pope Francis set for beatification". Aleteia — Catholic Spirituality, Lifestyle, World News, and Culture (kwa Kiingereza). 2018-06-22. Iliwekwa mnamo 2024-03-12.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.