Nenda kwa yaliyomo

Engy Sayed

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Engy Ahmed Atya Sayed (kwa Kiarabu: إنجي أحمد عطية سيد, alizaliwa tarehe 4 Septemba 1986), anayejulikana zaidi kama Engy Sayed, ni mchezaji wa soka kutoka Misri anayekipiga katika nafasi ya mshambuliaji kwa timu ya taifa ya wanawake ya Misri na klabu ya Ligi Kuu ya Wanawake ya Misri ya Al-Amerya.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Engy Sayed alizaliwa jijini Cairo, Misri, tarehe 4 Septemba 1986.[1][2] Alipata sapoti kubwa kutoka kwa familia yake inayopenda sana soka, na alikuwa akicheza mitaani pamoja na kaka zake na ndugu wengine. Alijitangaza kwa vilabu vya nje ya nchi kupitia jukwaa la YouTube. She scored twice in their qualifying campaign for the tournament, both goals being against Libya.[3]

Kazi ya klabu

[hariri | hariri chanzo]
Engy Sayed (kulia) wa Trabzon İdmanocağı akishambulia Beşiktaş J.K. (mweusi/mweupe katika mechi ya 2017–18 Ligi ya Kwanza ya Wanawake ya Uturuki ya ugenini.

Sayed alichezea klabu ya Wadi Degla SC yenye makao yake mjini Cairo kabla ya kuhamia Uturuki mnamo Novemba 2017 kujiunga na Trabzon İdmanocağı, ambao wanacheza katika Ligi ya Kwanza ya Soka ya Wanawake ya Uturuki (na jezi nambari 8).

Kwa sasa anaongoza klabu ya Misri Al-Amerya. Timu hiyo ilipoteza katika fainali za Kombe la FA la Wanawake la Misri mnamo 2023. Ni mara ya pili Sayed kupoteza katika fainali na klabu hiyo.[4]


  1. "Player Details: Engy Ahmed Atya Sayed". Türkiye Futbol Federasyonu. Iliwekwa mnamo 2017-12-30.
  2. "Confédéearion Africaine de Football 10th Edition Women's Afcon-Cameroon 2016 – 19.11.2016–03.12.2016 Media Start list" (PDF). CAF. Iliwekwa mnamo 2017-12-30.
  3. كمال, وليد (16 Desemba 2017). "مها، فريدة، إنجي... لاعبات كرة قدم مصريات حققن حلمهنّ بالاحتراف خارج مصر". Raseef 22 (kwa Kiarabu). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Agosti 2023. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Misri - Orodha ya Fainali za Kombe la Wanawake". RSSSF. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2023.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Engy Sayed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.