Emmanuel Okwi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Emmanuel Okwi, (alizaliwa Kampala, Uganda, 25 Disemba, 1992) ni mchezaji wa soka na anacheza klabu ya Simba S.C. na timu ya taifa ya Uganda. Taifa lake ni Uganda na anacheza nafasi ya kiungo.

Timu yake ya kwanza kucheza ni St. Henry kitovu College alipokuwa Uganda alikuwa anaichezea klabu ya SC Villa baada ya kuhamia Tanzania kuichezea Simba kwa US$ 40,000 ndani ya JANUARI timu ya Tunisia Etoile du Sahel na kusaini mkataba wa US$ 300,000 na kuvunja rekodi, Disemba 2013 alirudi SC Villa na Agosti 2014 alirudi Simba Sport Club na kusaini mkataba wa miezi (6) na mwaka 2015 alisaini mkataba wa miaka (5). Sasa hivi anaelekea katika timu ya Mamelod Sundown ya nchini Afrika ya Kusini.

Urefu wake ni mita 1.76. Alipata elimu yake huko St. Henry's College Kitovu. Amemuoa Florence Nakalegga.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emmanuel Okwi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.