Emma Goldman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Emma Goldman kunako mwaka wa 1910.

Emma Goldman (27 Juni 186914 Mei 1940) alikuwa akifahamika kama mfuasi wa utawala huria, kuanzia mwishoni wa karne ya 19 hadi katikati ya karne ya 20.

Imani[hariri | hariri chanzo]

Emma Goldman alikuwa mfuasi wa utawala huria (utawala huria ni nadharia ya siasa inayosema siasa na sheria havitakiwi), hivyo hakupenda serikali. Katika fikra zake alipendelea mtindo wa ukomunisti usiotia uzito kwa serikali na dola.

Aliamini kwamba watu wanapaswa wawe na maisha yao wenyewe, hivyo kila mtu atakuwa sawa na mwenziwe. Pia alikuwa mstari wa mbele katika kutaka haki sawa kwa wakinamama na alikuwa mtu wa kwanza kulilia haki za mashoga. Goldman pia alikuwa Mkanaji Mungu.

Goldman alikuwa akitetea sana mambo ya kutumia ubavu kwa ya imani ya kuleta mapinduzi halisi katika jamii, lakini baadaye alibadilisha kauli hiyo na kudai kwamba ubavu utatumikia katika kujilinda mwenyewe na si vinginevyo.

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Goldman alizaliwa katika mji wa Lithuania ya leo (wakati ule ilikuwa moja kati ya sehemu ya Urusi). Alipofikisha umri wa miaka kumi na saba akahamia mjini Rochester, New York akiwa pamoja na dada yake.

Mwanzo kabisa alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya kutengeneza nguo na akabahatika kuolewa na mfanyakazi mwenziye Bw. Jacob Kersner. Lakini ndoa yao haikudumu sana na Bi. Emma akaelekea zake mjini New York ambako huko ndiko alikokuja kuwa mmoja wa wafuasi wa utawala huria.

Pia akaja kuwa rafiki mkubwa wa Bw. Alexander Berkman (naye ni mfuasi wa utawala huria) na akamsaidia kupanga mpango wa kumwua Bw. Henry Clay Frick, tajiri anayesemekana kuwanyanyasa wafanyakazi wake. Lakini Bw. Berkman hakufanikiwa katika mpango huo badala yake akatumikia kifungo cha miaka kumi na minne jela, lakini Goldman hakupatiwa adhabu yoyote ile.

Goldman amekumbana na matatizo kibao ya kisheria. Mnamo mwaka wa 1893, alihukumiwa kwa kosa la kuanzisha mzozo na akatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. Kunako mwaka wa 1901, Emma alitiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusishwa na njama za kuuawa kwa rais wa 25 wa Marekani Bw. William McKinley, lakini akakutanika kuwa hana kosa na tuhuma hizo.

Mnamo kwa wa 1916 alitumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kutoa taarifa za siri za sehemu ya kuzalishia watu (ambapo kwa kipindi hicho ilikuwa ikihesabia kuwa kama kosa la jinai). Mnamo mwaka wa 1917 alikamatwa na kutiwa ndani kwa kosa la kutokubaliana na swala la kuanzisha Vita ya Kwanza ya Dunia.

Mnamo mwaka wa 1919, Goldman na Berkman walifukuzwa nchini Marekani, na kurudi kwao Urusi kwa sababu serikali ya Marekani ilikuwa ikiwafikiria kuwa watu hao ni hatari sana kwa taifa lao hivyo warudishwe makwao haraka iwezekanavyo. Baada ya kurudi huko, na Mapinduzi ya Urusi yakawa yameshatokea, hivyo Goldman akawa na imani kwamba sasa Urusi huenda ikawa sehemu nzuri.

Matokeo yake akawa anadai kwamba mapinduzi ya Urusi hayakuwa mazuri kama vile alivyokuwa akifikiria na kusema kwamba akina Bolsheviki waliwafanyia danganyatoto watu wengi wa nchini Urusi. Alifikiria kwamba Bolsheviki walikuwa watu wa kupenda kudhibiti watu kwa nguvu zaidi. Pia Goldman aliuchukia sana Umoja wa Kisovyeti kwa kuwaweka ndani wanaharakati wenzake wa utawala huria kwa kosa la kutokubaliana na watu hao wanaojiita wanautawala huria.

Emma na Berkman waliondoka nchini Urusi baada ya miaka miwili na Goldman akawa anaishi katika sehemu nyingi za nchi za Ulaya, ikiwemo Uingereza na Ufaransa. Mnamo mwaka wa 1936 alielekea zake nchini Hispania kwenda kuwasaidia wanautawala huria wenziye dhidi ya utawala wa kimabavu wakati ule wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispani.

Emma alifariki dunia mnamo tarehe 14 ya mwezi wa Mei katika mwaka wa 1940, kwa ugonjwa wa kupooza. Alizikwa karibu kidogo na mji wa Chicago.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]