Emile Heskey
Emile William Ivanhoe Heskey (alizaliwa 11 Januari 1978) ni mchezaji wa zamani wa soka la kulipwa kutoka Uingereza ambaye kwa sasa anahudumu kama mkuu wa maendeleo ya soka wa Timu ya Wanawake ya Leicester City
Akiwa mchezaji, Heskey alicheza katika nafasi ya mshambuliaji. Katika maisha yake ya soka yaliyodumu kwa miaka 18, alicheza zaidi ya mechi 500 katika Ligi ya Soka na Ligi Kuu ya Uingereza, pamoja na kuiwakilisha timu ya taifa ya Uingereza katika mashindano ya kimataifa.
Pia aliwahi kucheza nchini Australia, ambako aliichezea klabu ya Newcastle Jets inayoshiriki A-League.
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Heskey alizaliwa katika jiji la Leicester, katika kaunti ya Leicestershire, nchini Uingereza, akiwa anatoka katika familia yenye asili ya Antigua.
Baba yake, Tyrone Heskey, alikuwa akisimamia usalama wa vilabu vya usiku katika jiji la Leicester.
Heskey alisoma katika Shule ya Jiji la Leicester, iliyoko Evington, Leicester. [1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.liverpoolfc.com/info/emile-heskey
- ↑ https://web.archive.org/web/20150919052356/http://www.fifa.com/fifa-tournaments/players-coaches/people=177656/index.html
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Emile Heskey kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |