Emelia wa Kaisarea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Emelia wa Kaisarea alikuwa mke wa mhubiri maarufu Basili Mzee huko Caesarea Mazaca. Wote wawili walijulikana kwa imani yao (Basili Mkuu, Oratio 43.4, PG 36. 500B).

Familia yao ilikuwa na watoto 10, waliosaidiwa malezi na bibi yao, Makrina Mzee. Babu yao alikuwa mfiadini. Wote wawili wanaheshimiwa kama watakatifu, kama vile Basili Mkuu na watoto wengine 4: Makrina Kijana aliyekuwa mmonaki, Petro wa Sebaste aliyekuwa askofu na mwanateolojia huko Armenia, Naukratio aliyekuwa mkaapweke, na Gregori wa Nisa ambaye alifanywa na Basili kuwa askofu wa mji huo akaandika vitabu bora kuhusu teolojia na maisha ya Kiroho.

Alifariki tarehe 30 Mei 375.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhhimishwa hasa siku ya kifo chake au nyingine.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Emelia wa Kaisarea kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.