Nenda kwa yaliyomo

Elizabeti wa Utatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha yake halisi kama mtawa.
Élisabeth Catez akiwa msichana mwenye umri wa miaka 20.

Elizabeti wa Utatu, O.C.D. (Avord, Farges-en-Septaine, Ufaransa, 18 Julai 1880 - Dijon, Ufaransa, 9 Novemba 1906) ni jina la kitawa la Élisabeth Catez, anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.

Tangu utotoni alitafuta na kukazia macho ya moyo fumbo la Utatu Mtakatifu, na kupitia tabu nyingi, akiwa bado kijana alifikia alivyotamani kwenye upendo, mwanga na uzima[1].

Alipata umaarufu kwa maendeleo ya kiroho katika maisha yake yaliyofichika ndani ya monasteri ya Wakarmeli Peku[2], hasa baada ya kung'amua fumbo la uwemo wa Utatu Mtakatifu ndani ya roho yake[3].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 25 Novemba 1984; Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 16 Oktoba 2016.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Novemba[4].

Sala yake

[hariri | hariri chanzo]

Ee Mungu wangu, Utatu, ninayekuabudu, unisaidie nijisahau kabisa ili nikukazie macho wewe bila ya kubadilika na kwa utulivu, kama kwamba roho yangu ingekuwa tayari katika uzima wa milele.

Kisiwepo chochote cha kuvuruga amani yangu wala cha kunitoa nje yako, wewe usiyebadilika, uliye wangu; bali kila nukta nizidi kuzama katika vilindi vya fumbo lako!

Tuliza roho yangu; uifanye iwe uwingu wako, makao yako unayoyapenda zaidi na mahali pa pumziko lako. Humo nisikuache kamwe peke yako; bali niwemo mzima, mwenye kukesha na kutenda kwa imani yangu, mwenye kuzama katika kuabudu, mwenye kujiachilia kikamilifu kwa utendaji wako, Muumba.

Ee Kristo mpendwa wangu, uliyesulubiwa kwa upendo, nataka kuwa bibiarusi wa moyo wako, nataka kukujaza utukufu, nataka kukupenda hadi kufa kwa upendo! Lakini nahisi unyonge wangu wote: hivyo nakuomba uwe vazi langu, ulinganishe matendo yote ya roho yangu na yale ya roho yako, unizamishe ndani mwako, uenee ndani yangu, ushike nafasi yangu, ili maisha yangu yawe kioo cha maisha yako tu. Njoo ndani mwangu ili uabudu, ufidie, uokoe.

Ee Neno wa milele, Neno wa Mungu wangu, nataka kutumia maisha yangu kukusikiliza, nataka kuwa msikivu kabisa kwa mafundisho yako, nijifunze yote kwako, halafu katika usiku wa roho, katika utupu, katika unyonge nataka kukukazia macho daima na kubaki chini ya uangavu wako mkuu. Ee nyota yangu ninayoiabudu, unichanganye hata nisiweze tena kukwepa mng’ao wako.

Ee moto unaoteketeza, Roho wa upendo, ushuke ndani yangu ili katika roho yangu itokee aina ya umwilisho wa Neno! Niwe kwake mwendelezo wa ubinadamu wake ambapo aweze kutekeleza upya fumbo lake.

Nawe Baba uniinamie mimi kiumbe chako maskini, unifunike kwa kivuli chako, usione ndani yangu kitu kingine isipokuwa mpenzi wako uliyependezwa naye sana.

Enyi watatu wangu, yote yangu, heri yangu, upweke usio na mipaka, upana ambao napotea ndani yake, najiachilia kwenu kama mateka. Mzame ndani mwangu ili nami nizame ndani mwenu, wakati ninapongojea kuja kutazama katika mwanga wenu kilindi cha ukuu wenu[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/76725
  2. Of that experience as a professed religious she wrote in a letter: "I can't find words to express my happiness. Here there is no longer anything but God. He is All; He suffices and we live by Him alone" (Letter 91).
  3. "Blessed Elizabeth of the Trinity". Discalced Carmelites. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-08. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Martyrologium Romanum
  5. Order of Carmelites, Holy Trinity, Whom I Adore Ilihifadhiwa 8 Novemba 2019 kwenye Wayback Machine., accessed 8 November 2019

Maandishi yake

[hariri | hariri chanzo]
  • Elizabeth of the Trinity. Complete Works. 2 vol. Trans. Alethia Kane and Anne Englund Nash. Washington, DC: ICS Publications, 1984, 1995.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.