Nenda kwa yaliyomo

Eliza Lucas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Elizabeth "Eliza" Pinckney (alizaliwa Lucas; 28 Desemba 1722 – 27 Mei 1793)[1] alikuwa mkulima kutoka Marekani.

Pinckney alibadilisha mfumo wa kilimo katika koloni la South Carolina, ambapo aliendeleza kilimo cha indigo kuwa moja ya mazao muhimu ya biashara. Kilimo na uchakataji wa rangi ya indigo vilichangia takriban theluthi moja ya thamani yote ya bidhaa zilizokuwa zikisafirishwa nje ya koloni hilo kabla ya Vita vya Mapinduzi ya Marekani.

Akiwa msimamizi wa mashamba makubwa matatu ya kilimo,[2] Pinckney alikuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa kikoloni.

  1. [(https://www.encyclopedia.com/women/encyclopedias-almanacs-transcripts-and-maps/pinckney-eliza-lucas-1722-1793) "Pinckney, Eliza Lucas (1722–1779)"], encyclopedia.com. Iliangaliwa tarehe 7 Februari 2024.
  2. Pearson, Ellen Holmes. [(http://www.teachinghistory.org/history-content/ask-a-historian/24098) Colonial Teenagers], teachinghistory.org. Iliangaliwa tarehe 13 Julai 2011.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eliza Lucas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.