El Hadj M'Hamed El Anka
El Hadj M'Hamed El Anka (Mei 20, 1907 – Novemba 23, 1978) pia anajulikana kama Hadj Muhammed Al Anka, El-Hadj M'Hamed El Anka, alichukuliwa kuwa mtaalamu wa muziki wa Kimapokeo wa Andalusia na muziki wa chaâbi wa nchini Algeria.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Mei 20, 1907, kwa jina Ait Ouarab Mohamed Idir Halo, katika Kasbah ya Algiers. Familia yake, Ait Ouarab, walitokea Taguersift karibu na Freha huko Kabylia, [1] [2] baba yake alikuwa Mohamed Ben Hadj Saîd, na mama yake alikuwa Fatma Bent Boudjemaâ.
Baba yake aliugua siku ya kuzaliwa kwake. Kwa hiyo mjomba wake alipaswa kusajili kuzaliwa kwake. Hapo lilitokea kosa la kurekodi jina lake sahihi baada ya mjomba wake kujitambulisha mbele ya msajili kwa kusema "Ana Khalou" ("Mimi ni mjomba wake" kwa Kiarabu ), na msajili aliandika "Halo" akma jina la mtoto. Hivyo akawa Halo Mohamed Idir kuanzia hapo.
Alisoma katika shule tatu kuanzia 1912 hadi 1918: madrasa ya Kurani (1912–1914), Brahim Fatah (katika Kasbah) kuanzia 1914–1917, na huko Bouzaréah hadi 1918.
Alipokuwa na umri wa miaka 11 alipokelewa katika bendi kama Tardji yaani mpiga ngoma ndogo. Kiongozi wa bendi alimfundisha pia mandola ambayo ni ala inayofanana na gitaa. Tangu mwaka 1928 alianza kurekodi diski kwa ajili ya ampuni ya Cplombia na pia kwa ajili ya vipindi vya redio.
1937 alisafiri Makka kwa ajili ya hajj . Baada ya kurudi alianza safari za tamasha za muziki katika Aljeria na Ufaransa. Mwaka 1945 alipewa nafasi ya kuongoza muziki kwenye redio Algiers na mtindo wake ulipendwa na wasikilizaji kama muziki wa chaabi, yaani ya muziki wa wananchi. 1955 alipewa nafasi ya kundisha muziki kama profesa kwenye chuo cha Algiers.
Kwa jumla El Hadj El Anka alitunga nyimbo 360 ( qaca' id ) akatoa diski zipatao 130
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Kitchell, Liza Parker (1998). The development of Kabyle song during the twentieth century (kwa Kiingereza). University of Wisconsin--Madison. uk. 52.
- ↑ Saadallah, Rabah (1981). El-Hadj M'hamed El-Anka: maître et renovateur de la musique "chaabi" (kwa Kifaransa). La Maison des Livres. uk. 28.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu El Hadj M'Hamed El Anka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |