Ejiro Amos Tafiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ejiro Amos Tafiri ni mbunifu wa mitindo kutokea Nigeria, ni mjasiriamali na mwanzilishi wa chapa ya Ejiro Amos Tafiri (EAT) ambayo ilianzishwa ili kukidhi mahitaji ya mitindo ya mwanamke wa kisasa.[1]

Maisha ya Awali na Kazi[hariri | hariri chanzo]

Tafiri alizaliwa katika jiji la Lagos.[1] Upendo wake kwa mitindo ulianza akiwa na umri wa miaka mitatu kupitia ushawishi wa bibi yake ambaye wakati huo alikuwa mshonaji wake.[2] Alitarajiwa na wazazi wake kusoma udaktari lakini alichagua mavazi na ubunifu katika Chuo cha Teknolojia cha Yaba.

Tafiri alianzisha chapa yake mnamo 2010.[1] Mnamo mwaka wa 2015, mkusanyiko wa kazi yake iitwayo The Madame ilionyeshwa katika Wiki ya Mitindo ya Native & Vogue Port Harcourt, Wiki ya Mitindo ya Dakar na Wiki ya Mitindo ya Kenya.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Kemi Amushan. Ejiro Amos Tafiri: The E. A. T. Brand. The Guardian. Iliwekwa mnamo 25 July 2016.
  2. Olamide Olanrewaju. My First encounter with fashion was at 3" - Fashion Designer. Pulse .ng. Iliwekwa mnamo 25 July 2016.
  3. Jennifer Obiuwevbi. Glam Overdose! Ejiro Amos Tafiri’s 2015 Luxury Resort Collection – “The Madame”. Bella Naija. Iliwekwa mnamo 25 July 2016.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ejiro Amos Tafiri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.