Nenda kwa yaliyomo

Edward Teller

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edward Teller (1908 - 2003) alikuwa mwanafizikia wa Hungaria. Anajulikana kama baba wa bomu la hidrojeni. Hata hivyo hakupenda hiyo sifa ya kuwa ndiye mvumbuzi wa bomu la hidrojeni. Maishani mwake Edward Teller anasemekana kuwa mwenye talanta kuu katika uwanja wa fizikia. Hata hivyo anajulikana pia kwa kuwa mtu mgumu sana wa kuelewana naye.

Masomo[hariri | hariri chanzo]

Edward Teller alizaliwa na Ilona aliyekuwa mcheza kinanda na Max Teller aliyekuwa wakili. Wazazi wake walikuwa Wayahudi.

Alisomea shule ya Fasori Lutheran Gymnasium. Sawa tu na wanafizikia wengine kama Albert Einstein na Richard Feynman, Edward Teller alichelewa kuongea japo alipoweza kuongea aliendelea kukaa mpweke huku akiyasuluhisha masuala ya hesabu.

Kati ya mwaka 1926 hadi 1928, Edward alisomea hisabati na kemia katika chuo kikuu cha Karlsruhe alipopata shahada ya uhandisi katika kemia.

Baada ya kusikiliza maongezi ya Herman Mark, Teller alibadili na kuanza kusoma somo la fizikia alilopata shahada ya PhD katika chuo cha Leipzig.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]