Eduardo da Silva
| Eduardo | |
Eduardo akiwa na Shakhtar Donetsk Mei 2011 | |
| Amezaliwa | 25 Februari 1983 Rio de Janeiro, Brazil |
|---|---|
| Urefu | 1.78 m |
Eduardo Alves da Silva (alizaliwa 25 Februari 1983), anayejulikana zaidi kama Eduardo au Dudu,[1][2] ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa kulipwa aliyecheza kama mshambuliaji katika klabu mbalimbali na pia katika timu ya taifa ya Kroatia.
Alianza safari yake ya soka katika klabu ya nyumbani kwao nchini Brazili ya Bangu Atlético Clube. Baadaye, alijiungu na timu ya vijana ya GNK Dinamo Zagreb ya nchini Kroatia. Alitolewa kwa mkopo kwa muda katika klabu ya NK Inter Zaprešić ya huko huko nchini Kroatia, ambapo alifunga mabao kumi katika mechi 15. Uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu akiwa na Dinamo Zagreb, ambapo aliounyesha alipofunga mabao 73 katika mechi 109 za ligi, ulivutia klabu ya Arsenal iliyomsajili kwa kiasi cha pauni milioni 7.5 mnamo mwaka 2007. Jeraha kubwa na la hatari la mguu lilivuruga kipindi chake cha kukaa Arsenal na, baada ya msimu mitatu na klabu hiyo, alihamia FC Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraini mwaka 2010.
Eduardo alichukua uraia wa Kroatia mnamo mwaka 2002 na alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa katika timu ya taifa ya Kroatia akitokea benchi kipindi cha pili kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ireland tarehe 16 Novemba mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 21. Alichaguliwa na kocha wa timu ya taifa Slaven Bilić kushiriki mashindano ya UEFA Euro 2012, na akachaguliwa tena na Niko Kovač kwa ajili ya kombe la dunia la FIFA la mwaka 2014. Akiwa amefunga mabao 29 kwa ajili ya Kroatia, Eduardo ni mchezaji wa tano kwa ufungaji wa mabao ya kihistoria katika nchi hiyo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Sportal.hr – Dudu ponovo strijelac! Arsenalu..., Sportal, nogomet, strani nogomet" (kwa Kikorasia). Vecernji.hr. 28 Novemba 2010. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sportal.hr – Dudu je uspio – zabio Arsenalu! (video i galerija), Sportal, nogomet, strani nogomet" (kwa Kikorasia). Vecernji.hr. 19 Oktoba 2010. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu wakimbizi au masuala ya ukimbizi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eduardo da Silva kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |