Nenda kwa yaliyomo

Edna P. Plumstead

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edna P. Plumstead (née Janisch; 15 Septemba 1903 - 23 Septemba 1989) alikuwa mwanahistoria wa paleobotania wa kutoka nchi ya Afrika Kusini, wa Taasisi ya Bernard Price ya Utafiti wa Paleontolojia, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg, mahali alipo hitimu mnamo 1924. Edna aliweka makazi Cape Town miaka saba ya kwanza ya maisha yake na hapo ndipo angechunguza na kupata maua ya porini kwenye Rasi ya Cape. Plumstead baadaye alifanya muunganiko wa maua ya porini na yale yale katika maeneo kama Australia na Amerika Kusini na hapo baadaye angetetea utelezi wa bara. Alianza kutetea nadharia ya utelezi wa bara kwenye mnamo wa miaka ya 1950 na watu wanamuelezea kama mmoja wa 'wanasayansi wakuu wa Afrika Kusini kwenye uwanja wa paleobotania na jiolojia ya Gondwana '. [1] Plumstead alipewa Nishani ya Chrestian Mica Gondwanaland na Jumuiya ya Jiolojia ya India, na akafanywa Mwanachama wa Jumuiya ya Kifalme ya Afrika Kusini .

Plumstead alomaliza masomo yake mwaka wa 1924 kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand na Shahada ya Kwanza ya Sayansi (Hons.) juu ya jiolojia na akachukua miadi na Idara ya Jiolojia. Tasnifu yake ya shahada ya uzamili ili pewa hushima kubwa sana na Jumuiya ya Jiolojia ya Afrika Kusini na hili likamfanya kuwa mpokeaji wa kwanza wa Nishani ya Corstorphine. Alijiunga na Taasisi ya Bernard Price mnamo wa 1965 kutoka Idara ya Jiolojia. Kipindi hicho alikuwa akisoma visukuku vya mimea vilivyokusanywa Antaktika, na polepole akaamini kwamba miamba ya mchanga ya umri huo huko Antaktika, Afrika Kusini, Amerika Kusini, India na Australia ilikuwa na visukuku vya mimea vinavyofanana kimsingi. Spishi hizi zilianzia mwishoni mwa Palaeozoic na kuendelea.

Japo hii ilikuwa kipindi kirefu kabla ya kukubalika kwa jumla kwa 'kuteleza kwa bara', tektoniki za plate na kuenea kwa sakafu ya bahari, watu baadhi waliona mimea ya visukuku vya Antaktika kama ushahidi wa mawazo kuelekeza kwa kuwepo kwa 'bara kubwa' la zamani, Gondwana . Miaka mitano mbeleni baada ya ushahidi wa palaeobotania kutangazwa kwa ulimwengu, James Kitching aliongeza ushahidi wa visukuku vya wanyama wenye uti wa mgongo kwenye mjadala huu alipojiunga na Kundi la Utafiti la Antaktika la Marekani kwenye ziara yake mnamo wa 1970, na kuziunganisha pamoja visukuku vya wanyama wenye uti wa mgongo sawa na vile alivyozoea kupata huko Karoo .

Kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Plumstead alifanya makazi Afrika Kusini, nchi ambayo nadharia ya Wegener ya kuteleza kwa Bara ilikuwa sahihi na ilifundishwa shuleni, ambayo ilikuwa tofauti na Amerika Kaskazini na Ulaya ambapo nadharia hiyo ilikuwa imekataliwa. Kutokana na hilo, aliathiriwa na dhana ya Wegener na akavutiwa sana na ukweli kwamba maisha ya nyuma duniani hayakusambazwa sawasawa, lakini kwamba yalikuwa yamegawanywa katika maeneo. Pamoja na hayo alijifunza juu ya uvumi wa bara la kale lililoitwa Gondwanaland na akaamua kujifunza zaidi kuihusu. Alifanya ugunduzi wake muhimu zaidi mwaka 1952, ambao ulikuwa ni uundaji wa Glossopteris, mmea wa Permian unaopatikana kila mahali wa Gondwana, na baadaye akawa mtaalamu wa jambo hilo. [2]

Kipindi uchunguzi wake unaendelea, alilinganisha mimea ya Kusini na Kaskazini mwa Ulimwengu, na ikasababisha yeye kugundua kwamba baadhi ya nchi, ikiwa ni pamoja na Afrika, Amerika Kusini, India, Australia na Antaktika zilikuwa na mimea kama hiyo hapo kipindi cha nyuma. Uchunguzi wake ulikuwa wa msingi kwa sababu ulitumika kama uthibitisho wa kuwepo kwa Gondwana . Tunaweza kusoma kuihusu katika kitabu chake "The Case for Continental Drift". [3]

Kwenye uchunguzi wake kulikuwa na maswali mawili ya msingi ambayo aliuliza na kujaribu kuyavavadua. La kwanza lilikuwa hili : “Kama nafasi ya mabara isingebadilika, je, jenasi moja na hata spishi za mimea zingewezaje kwenenda mashariki, magharibi na kusini kuvuka bahari kubwa ambazo sasa zinazitenganisha, japo zimeshindwa kufika Amerika Kaskazini, Ulaya na Asia kwa njia rahisi?” Swali la pili lilikuwa hili: “Kama maeneo ya hali ya hewa yalikuwa sawa, tunawezaje kuelezea ukweli kwamba mimea ya visukuku ya India ya peninsula inafanana kwa karibu, na mara nyingi inaendana na ile ya Australia, Afrika kusini mwa Sahara, Argentina na Brazil japo zaidi ya yote, na ile inayopatikana humo katikati ya Antaktika katika 86˚S ambapo leo hakuna mmea wa mishipa ungeweza kuishi?” [4]

Plumstead pia alichangia nafasi kwenye usambaaji wa nadharia ya uhamaji kwani alitoa taarifa nzuri zaidi juu ya Glossopteris ambazo zilichangia kwenye tafsiri na uelewa wa mgawanyiko wa Gondwana . Akawa sauti halisi ya uhamaji.

Kazi yake, pamoja na ile ya Wegener, du Toit na Martin ilimpa msaada Warren Hamilton, ambaye alikuwa mshabiki wa nadharia ya kuteleza kwa bara, kukuza nadharia yake juu ya uhamaji ambayo kisha akaitumia Amerika. [3]

Plumstead alikuwa mtu wa kwanza kutoa maelezo juu ya miundo ya ajabu yenye rutuba ya mmea wa Glossopteris inayopatikana kwenye uhusiano wa kikaboni na majani. Pamoja na hayo, kipindi cha utafiti wake, kwenye mapitio yake ya "Paleobotany huko Antaktika"; alifikia mwaafaka kwamba ni lazima kwamba ushahidi kutoka Antaktika unahitaji maelezo ya kifiziolojia yanayowezekana zaidi kuliko yoyote yaliyotolewa hapo nyuma, na inaonekana kuridhishwa na kukubalika kwa aina fulani ya mkondo wa bara. [ <span title="This claim needs references to reliable sources. (April 2019)">nukuu inahitajika</span> ]

Akiwa kama mwanasayansi wa paleobotanist pia, alijifunza juu ya visukuku na alipata shauku sana na ya jinsi visukuku vya spishi moja vilivyoishia katika mabara tofauti - anamtumia Gondwana kuelezea hili. Machapisho yake juu ya mkondo wa bara zilijadiliwa sana na ni muhimu kwa maendeleo yake mwenyewe kwenye utafiti wake wa visukuku. Warren Hamilton, ambaye alikuwa mshabiki wa uhamaji na alikwenda Afrika kutafuta ushahidi wa kuunga mkono nadharia yake, huku akiwa Afrika alisoma kazi ya Plumstead - ilikuwa shukrani kwake (na watu wengine wawili) kwamba aliweza kuthibitisha nadharia yake ya uhamaji kuwa kweli. Plumstead alitoa mchango mkubwa katika uelewa wa Glossopteris, akitoa ushahidi muhimu unaothibitisha tafsiri ya uhamaji ya Gondwana. Kupitia kazi na utafiti mwingi wa Plumstead, wanasayansi wengine wameweza kuthibitisha nadharia zao wenyewe ambazo zimetusaidia kujua kuhusu ulimwengu kama ulivyo leo. [5]

Orodha ya sehemu ya machapisho

[hariri | hariri chanzo]
  • EP Plumstead, 'Maelezo ya jenasi mbili mpya na spishi sita mpya za matunda zinazotokana na majani ya Glossopteris kutoka Afrika Kusini', Trans Geol Soc S Afr, 55 (1952), 281–328
  • EP Plumstead, 'Mauaji ya jinsia mbili yanayotokana na majani ya Glossopteris kutoka Afrika Kusini. Palaeontographica, 100B (1956),1–25
  • Edna P. Plumstead, Uzalishaji wa matunda wa jinsia mbili unaotokana na majani ya Glossopteris kutoka Afrika Kusini (Stuttgart, E. Schweizerbart, 1956)
  • Edna P. Plumstead, Makaa ya Mawe Kusini mwa Afrika (Johannesburg: Witwatersrand University Press, 1957)
  • Edna P. Plumstead, Kuhusu Ottokaria, uundaji wa matunda wa Gangamopteris (Johannesburg) : Hortors Ltd., [1957?])
  • EP Plumstead, 'Matokeo zaidi ya Glossopteridae na uainishaji wa muda unaotegemea wao', Trans Geol Soc S Afr, 61 (1958), 52–74
  • Edna P. Plumstead na R Kraűsel. Mimea ya visukuku vya Antaktika (London: Kamati ya Safari ya Kuvuka Antaktika, 1962)
  • Edna P. Plumstead, Miaka Elfu Tatu Milioni ya Maisha ya Mimea Afrika (Johannesburg: Jumuiya ya Jiolojia ya Afrika Kusini, 1969)
  • Edna P. Plumstead, 'Karatasi ya pamoja kuhusu Gondwana paleobotany' (1970)
  • Edna P. Plumstead, Mkusanyiko mpya wa visukuku vya mimea kutoka Milorgfjella, Dronning Maud Land (Cambridge Utafiti wa Antaktika wa Uingereza, 1975)
  • Vitabu vyake vilivyochapishwa:
  • Mimea ya Fossil ya Antarctica-toleo la 1 lilichapishwa kwa Kiingereza mnamo 1962
  • Mchoro wa Sehemu ya Ramani Rahisi za Jiolojia - matoleo 8 yaliyochapishwa kwa Kiingereza kati ya 1938 na 1946
  • Jiolojia-toleo la 1 lililochapishwa kwa Kiingereza mnamo 1962
  1. Maguire, J M (Januari 1990). "Dr. Edna P. Plumstead FRSSAf". Transactions of the Royal Society of South Africa. 47 (3): 355–357. doi:10.1080/00359199009520247.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Frankel, Henry R (2012). The Continental Drift Controversy: Wegener and the early Debate. Cambridge University Press.
  3. 1 2 Frankel, Henry R (2012). The Continental Drift Controversy: Wegener and the early Debate. Cambridge University Press.Frankel, Henry R (2012). The Continental Drift Controversy: Wegener and the early Debate. Cambridge University Press.
  4. Edna P. Plumstead and R Kraűsel (1962). Fossil floras of Antarctica. London: Trans-Antarctic Expedition Committee.
  5. Frankel, Henry R. (2016-12-12). The Continental Drift Controversy: Volume 1, Wegener and the Early Debate (kwa Kiingereza). Cambridge University Press. ISBN 9781316616048.