Edith WeUtonga
Mandhari
| Edith Weitonga | |
|---|---|
| | |
| Jina Kamili | Edith Waitonga |
| Jina la kisanii | Edith Weitonga |
| Nchi | Zimbabwe |
| Alizaliwa | 22 Aprili 1979 |
| Aina ya muziki | Rhumba |
| Kazi yake | Musical artist 2 |
| Miaka ya kazi | 16 |
Edith WeUtonga (alizaliwa tarehe 22 Aprili 1979), ni msanii wa muziki wa Afro-jazz na muziki wa asili kutoka Zimbabwe. Pia ni mpiga gitaa la besi, mtunzi wa nyimbo, mwigizaji na mwalimu wa muziki. Alizaliwa mjini Kadoma, uliopo takribani kilomita 166 kusini-magharibi mwa Harare kwa barabara.
Akiwa na asili ya Malawi na kukulia mjini Bulawayo, Edith huimba kwa lugha nne tofauti, ambazo ni Kishona, Kichichewa, Kindebele na Kiingereza. Bendi yake inaitwa Utonga, neno linalomaanisha mapambazuko. Ni miongoni mwa wapiga gitaa wachache wa besi nchini Zimbabwe ambao pia ni waimbaji wakuu wa bendi. Mbali na besi, pia anapiga gitaa la akustiki, mbira, na ngoma.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Samukange, Tinotenda (12 Mei 2015). "Edith WeUtonga speaks on her life". News Day. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-26. Iliwekwa mnamo 24 Septemba 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Edith WeUtonga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |