Edgar Peña Parra
Mandhari
Edgar Robinson Peña Parra (alizaliwa 6 Machi 1960) ni askofu mkuu wa Venezuela wa Kanisa Katoliki. Papa Fransisko alimteua kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Vatikani tarehe 15 Agosti 2018, kuanza rasmi tarehe 15 Oktoba, na kumfanya kuwa mtu wa juu zaidi kutoka Venezuela katika Curia ya Kirumi.
Alijiunga na diplomasia ya Vatikani mwaka 1993, akihudumu kama Balozi wa Papa (Apostolic Nuncio) nchini Pakistan kutoka 2011 hadi 2015 na nchini Msumbiji kutoka 2015 hadi 2018. Yeye ni Mvenezuela wa kwanza kuhudumu kama balozi wa Papa.
Anazungumza kwa ufasaha Kihispania, Kiitalia, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, na Kiserbokroatia.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ García, Pedro M. (15 Agosti 2018). "El venezolano Edgar Peña Parra, sustituto de la Secretaría de Estado vaticano". Vida Nueva (kwa Kihispania). Iliwekwa mnamo 15 Agosti 2018.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |