Nenda kwa yaliyomo

Edem Atovor

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Edem Atovor (alizaliwa 10 Aprili, 1994) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa wanawake kutoka nchini Ghana. Amechezea klabu ya mpira mbalimbali ikiwa ni pamoja na Lady Strikers, Maccabi Kishronot Hadera FC pamoja na timu ya taifa ya wanawake ya Ghana, na kwa sasa anakipiga katika klabu ya mpira ya Hapoel Petah Tikva nchini Israeli.[1]

Atovor alianza taaluma yake ya soka mwaka 2005 akiwa na klabu ya Ghatel Ladies mjini Cape Coast. Mwaka 2007 alipandishwa kujiunga na timu ya wakubwa. Baada ya kucheza kwa miaka mitatu katika ligi ya juu kabisa ya wanawake nchini Ghana akiwa na Ghatel Ladies, alihamia Cape Coast Vodafone Ladies.

Baada ya msimu mmoja katika Ligi ya Wanawake ya Kanda ya Tatu akiwa na Vodafone Ladies, mwaka 2011 alihamia kwa wapinzani wa jiji hilo, Lady Strikers. Hata hivyo, hakufanikiwa kuendana na timu hiyo, hivyo mwanzoni mwa msimu wa 2012 alihamia kwa mkopo kutoka Lady Strikers kurejea katika klabu yake ya zamani ya vijana, Cape Coast Ghatel Ladies.

  1. Ghana – CAN féminin : La présélection – Afrik11.com Archived 2011-11-22 at the Wayback Machine
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edem Atovor kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.