Eberechi Eze
| Eberechi Eze | |
| Amezaliwa | 29 Juni 1998 Greenwich, Greater London, Uingereza |
|---|---|
| Nchi | Uingereza |
| Mwajiri | Arsenal |
| Urefu | 1.78 m |
Eberechi Oluchi "Ebere" Eze (alizaliwa 29 Juni 1998) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Uingereza anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji katika klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza na timu ya taifa ya Uingereza.[1][2]
Wakati anakua, alipitia vyuo mbalimbali vya soka nchini Uingereza, Eze alianza kazi yake ya soka la wakubwa katika ligi ya daraja la kwanza akiwa na klabu ya Queens Park Rangers mwaka 2016. Mafanikio yake makubwa yalikuja katika msimu wa 2019–20, ambapo alifunga mabao 14 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mwaka wa klabu hiyo. Baadaye alisajiliwa na klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Crystal Palace, ambapo alicheza mechi zaidi ya 150 na kufunga bao pekee katika fainali ya kombe la FA ya mwaka 2025 iliyoiwezesha klabu hiyo kutwaa taji lake kuu la kwanza kabisa. Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii ya FA ya mwaka 2025 akiwa na Palace, alisajiliwa na klabu ya utotoni mwake ya Arsenal kwa ada ya pauni milioni 67.5, ambapo alishinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza na kufika fainali ya ligi ya mabingwa ya ulaya ya mwaka 2026 katika msimu wake wa kwanza.
Aliwahi kuwa mchezaji wa timu za taifa za vijana za Uingereza, Eze aliichezea timu ya taifa ya wakubwa kwa mara ya kwanza mwaka 2023, na baadaye aliisaidia nchi yake kushika nafasi ya pili katika mashindano ya ubingwa wa mpira wa miguu wa Ulaya wa UEFA 2024, pamoja na kushika nafasi ya tatu katika kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Why Eze WONT be stopped by injuries and rejections (kwa English). Rising Ballers. 4 Februari 2022. Tokeo mnamo 0:20. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2022 – kutoka YouTube.
{{cite AV media}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link) - ↑ How to pronounce Eberechi Eze (kwa English). Crystal Palace F.C. 28 Agosti 2020. Tokeo mnamo 0:00. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2022 – kutoka Facebook.
{{cite AV media}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Eberechi Eze kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |