Nenda kwa yaliyomo

Ebele Okoye

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ebele Okoye


Ebele Okoye
Amezaliwa 6 Oktoba 1969
Nigeria
Nchi Marekani
Majina mengine Omenka Ulonka
Kazi yake Mchoraji

Ebele Okoye (kuzaliwa Onitsha, Anambra State, 6 Oktoba 1969) ni mchoraji na muhuishaji Mmarekani mwenye asili ya Nigeria [1] akiwa Cologne, Ujerumani toka mwaka 2000.

Okoye alisoma Sanaa akibobea katika ubunifu wa grafiki na uchoraji katika chuo cha Usimamizi na Teknolojia kilichopo Enugu kutoka mwaka 1985 mpaka 1989. Alipowasili Ujerumani mwaka 2000, alifanya mpango wa wageni katika chuo cha University of Cologne, ambayo aliacha na kwenda kujisajili kwenye Muundo wa Mawasiliano katika chuo cha Applied Sciences kilichopo Düsseldorf.

Kutoka mwaka 2003 mpaka mwaka 2004, Alipitia mafunzo ya Jadi ya matengenezo ya katuni kwa kutumia 2D katika chuo cha Internationale Filmschule Köln. Anaongea kwa ufasaha lugha za Igbo, Kiingereza, na Kijerumani.[2]

Ebele Okoye anafanya kazi ya Sanaa na media na amekuwa akionesha kazi zake katika maonesho ya mtu mmoja nay a kikundi angalia chini). Ni muanzilishi wa Shrinkfish Media Lab,[3] a production company based in Abuja.[4]

Filamu ya Okoye ya 2015 iitwayo The Legacy of Rubies ilikua moja kati ya filamu mbili zilizofunga mwaka 2015 katika sherehe za Silicon Valley African Film .[5] Mwaka huo filamu yake hiyo ilishinda Africa Movie Academy Award kwa uhuishaji bora. Okoye alisema kua "Sijatengeneza filamu hii ili kufukuzia tuzo," katika hotuba yake ya kupokea tuzo Afrika ya Kusini. "Nimetengeneza hii filamu , ili kuhamasisha kila muhuishaji wa Kiafrika anayetaka kutengeneza filamu za uhuishaji." Filamu ya The Legacy of Rubies ilioneshwa kwa mara ya kwanza nchini Canada mwaka 2016 pale Toronto Black Film Festival .[6][7]

Mwaka 2016 alitangaza mipango ya kutengeneza filamu ya kipengele kirefu, Akigusia kua inaweza kua “kama Chronicles of Narnia naPocahontas (1995 film)|Pocahontas zikiunganishwa Pamoja."[8]

Mradi wake wa mwaka 2007 Anna Blume, kulingana na shairi la 1919 la Kurt Schwitters,[9]alishinda tuzo ya Robert Bosch Foundation Promotional Prize Kwa uhuishaji.[10] Okoye ameshinda tuzo mbili za Africa Movie Academy Awards, kwa filamu ya The Lunatic (2008) na kwa filamu ya The Legacy of Rubies (2015).

  1. "Niyi Akinmolayan, Stanlee Ohikhuare gear up for 'Animation film day'". Pulse Nigeria (kwa American English). 13 Novemba 2018. Iliwekwa mnamo 29 Januari 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Nkiru Nzegwu, "Immigration and African Diaspora Women Artists" in Isidor Okpewho and Nkiru Nzegwu, eds., The New African Diaspora (Indiana University Press 2009): 324. ISBN 9780253003362
  3. Adebimpe Adebambo, "Ebele Okoye: Charting New Territory" Archived 10 Aprili 2021 at the Wayback Machine. Omenka Online (28 March 2016).
  4. "Ebele Okoye" Great Women Animators database (2016).
  5. "The 6th Annual Successful Silicon Valley African Film Fest Does It Again" Bay View (15 November 2015).
  6. Alexe Louisa, "Toronto Black Film Festival (TBFF) Announces Line-up" Toronto Black Film Festival (20 January 2016).
  7. | Ebele Okoye is a German 2D animation film maker of Nigerian descent based in Berlin.
  8. "Animation Filmmaker Ebele Okoye Goes Feature" The Nation (2016).
  9. "Animated Film: Anna Blume" Archived 4 Oktoba 2018 at the Wayback Machine. Robert Bosch Stiftung, 2007 Winners.
  10. "Biography: Ebele Okoye" Archived 23 Februari 2022 at the Wayback Machine., Directors, Africa Film Trinidad Tobago.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ebele Okoye kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.