Nenda kwa yaliyomo

Dyson sphere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nadharia ya Dyson Swarm

Dyson sphere ni muundo wa kinadharia unaozunguka nyota, uliobuniwa kwa lengo la kunasa asilimia kubwa ya nishati inayozalishwa na nyota hiyo.[1]

Wazo hili liliibuliwa kama jaribio la kifikra na mwanafizikia Freeman Dyson mnamo 1960, ambaye alikiri mwenyewe alipata msukumo wa wazo hilo kutoka katika riwaya ya sayansi ya kubuni (fiction science novel) Star Maker (1937) iliyoandikwa na Olaf Stapledon.[2]

Aina ya msingi ya Dyson sphere ambayo Dyson alipendekeza ni Dyson Swarm mkusanyiko wa miundo huru, kama satelaiti au vikusanyanuru, vinavyozunguka nyota katika obiti mbalimbali ili kukusanya nishati.[3]

Dyson alieleza kwamba wazo la ganda gumu (solid shell) linalozunguka nyota , ambalo mara nyingi huonyeshwa katika fasihi na michoro ya kisayansi, haliwezekani kimakanika kwa sababu ya changamoto za mvutano na upatikanaji wa nyenzo zinazoweza kuhimili shinikizo.[4]

Wazo la Dyson sphere pia linatumika katika utafiti wa uwepo wa viumbe wenye akili nje ya Dunia (ETI), kwani mfumo huo ungetarajiwa kutoa mionzi ya infra-red (joto) isiyo ya kawaida. Mwaka 2015, nyota ijulikanayo kama KIC 8462852 (inajulikana pia kama Nyota ya Tabby) ilizua mjadala mkubwa kutokana na mabadiliko yake yasiyo ya kawaida ya mwanga, na baadhi ya wanasayansi walipendekeza uwezekano wa miundo ya aina ya Dyson sphere kabla ya nadharia za asili kuthibitishwa[5][6]

Dhima ya Dyson sphere imekuwa maarufu katika kazi za sanaa na fasihi za sayansi ya kubuni, imeonekana katika kazi mbalimbali, ikiwemo vipindi vya televisheni kama Star Trek: The Next Generation..[7]

  1. Dyson, Freeman J. (1960). "Search for Artificial Stellar Sources of Infrared Radiation" (Tafuta Vyanzo Bandia vya Nyota vya Mionzi ya Infra-Red). Science. 131 (3414): 1667–1668.
  2. Kardashev, Nikolai (1985). On the Inevitability and the Possible Structures of Supercivilizations (Juu ya Kuepukika na Miundo Inayowezekana ya Ustaarabu Mkuu). Uk. 497–504.
  3. Dyson, F. J.; Maddox, J.; Anderson, P; Sloane, E. A. (1960). "Letters and Response, Search for Artificial Stellar Sources of Infrared Radiation". Science. 132 (3421): 250–253.
  4. Westfahl, Gary (2021). "Artificial Worlds". Science Fiction Literature through History: An Encyclopedia. ABC-CLIO. Uk. 135–136.
  5. Andersen, Ross (13 October 2015). "The Most Mysterious Star in Our Galaxy". The Atlantic.
  6. Boyajian, Tabetha S.; et al. (2018). "The First Post-Kepler Brightness Dips of KIC 8462852". The Astrophysical Journal. 853 (1). L8.
  7. Hadhazy, Adam (October 30, 2020). "Could We Build a Dyson Sphere?". Popular Mechanics.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dyson sphere kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.