Nenda kwa yaliyomo

Durba Mitra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Durba Mitra Ni mhadhiri wa Chuo kikuu cha Harvard na mwanahistoria kutoka Marekani. Ameandika kuhusu wanawake, jinsia na historia ya jamii. Mwaka 2018 alichaguliwa kuwa mwalimu msaidizi katika Taasisi ya Radcliffe, na baadaye akawa mwalimu wa kwanza wa kudumu katika masomo ya wanawake na jinsia. [1][2][3][4]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Mama yake Mitra ni mhamiaji kutoka India aliyewamlea Mitra na kaka yake akiwa peke yake. Alifanya kazi na kusoma huku akiwalea watoto wake bila mume. Alijitahidi kuwapa uhuru na kuwahimiza kujitambua, alimpa Mitra hamasa ya kuchunguza fursa mbalimbali za maisha, jambo lililomfanya Mitra kuwa na mtazamo wa kipekee kuhusu maisha..

Elimu na taaluma

[hariri | hariri chanzo]

Mitra alianza masomo yake akiwa na ndoto za kuwa daktari, lakini baadaye aligeuka na kuanza kujifunza masuala ya historia, jinsia, na wanawake. Alimaliza PhD mwaka 2013, alifanya utafiti wa historia ya India wakati wa ukoloni. Sasa anafundisha chuo kikuu Harvard na ni mhariri wa jarida la historia ya mawazo.

  1. "Challenging the Norms: Durba Mitra Comes to Harvard | Magazine | The Harvard Crimson". www.thecrimson.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-16.
  2. mbolot@harvardmag.com (2018-09-07). "Durba Mitra studies gender in South Asia | Harvard Magazine". www.harvardmagazine.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-16.
  3. "Tools for Success | Emory University | Atlanta GA". gs.emory.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-16.
  4. "WGS Hires First Full-Time Professor | News | The Harvard Crimson". www.thecrimson.com. Iliwekwa mnamo 2024-05-16.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Durba Mitra kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.