Duffer Brothers
| Matt and Ross Duffer | |
|---|---|
Matt Duffer akiwa upande wa kushoto, na Ross Duffer upande wa kulia, wote wameketi nyuma ya meza yenye kadi za majina mbele yao na wakitazama upande wa kushoto wa mtazamaji, huku nyuma kukiwa na bango la San Diego Comic-Con. | |
| Amezaliwa | 15 Februari 1984 |
| Elimu | Chapman University (BFA) |
| Kazi yake |
|
| Miaka ya kazi | 2005–hadi sasa |
| Ndoa | Leigh Janiak (m. 2015–2024) (Ross) |
Matt Duffer na Ross Duffer (maarufu kama Duffer Brothers; walizaliwa 15 Februari 1984) ni waandishi, waongozaji na watengenezaji wa filamu kutoka Marekani. Ndugu hao ni mapacha wanaofanana na wanafanya kazi na miradi yao yote kwa pamoja[1]. Wanajulikana zaidi kama waandaaji, na wazalishaji wa tamthilia ya kutisha ya Netflix inayofahamika kama Stranger Things (2016-2025), Pia waliandika na kuaandaa filamu ingine ya kutisha inayoitwa Hidden (2015).Pia waliandaa tamthilia ya kisayansi Wayward Pines(2015-2016). Ndugu hao ni waanzilishi wa kampuni ya uzalishiji wa filamu iitwaje Upside Down Pictures ambayo inashirikiana na Netflix[2].
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya ndugu hao kuandika na kuandaa filamu fupi fupi, waliandika skripti ya filamu iitwayo "Origin" ambayo iliwapa umaarufu. Na baadae skripti yao ya filamu ya kutisha iitwayo "Hidden" iliyotolewa mwaka 2015[3]. Na baada ya hapo ndugu hao waliajiriwa na Fox kama waandishi na waongozaji wa tamthilia ya Wayward Pines. Mpaka kufikia mwaka 2024, ni wazalishaji wakuu wa tamthilia ya Netflix iitwayo The Boroughs[4].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Dymond, Erica Joan (2022). "Misnomers and Contemporizations". Reclaiming the Tomboy: 159–184. doi:10.5040/9781978722095.ch-008.
- ↑ Mollet, Tracey (2019-03-01). "Looking through the upside down: Hyper-postmodernism and trans-mediality in the Duffer Brothers' Stranger Things". Journal of Popular Television, The. 7 (1): 57–77. doi:10.1386/jptv.7.1.57_1. ISSN 2046-9861.
- ↑ Fernandez, Tony (2015-02-01). "Setting the Foundation With the Bricks From Others: Advice for Recent Grads". The Way Ahead. 11 (01): 3–3. doi:10.2118/0115-003-twa. ISSN 2224-4522.
- ↑ Baker, Djoymi; Balanzategui, Jessica; Sandars, Diana (2023-05-24), "The Haunted Nostalgia of The Dark Crystal: Age of Resistance", Netflix, Dark Fantastic Genres and Intergenerational Viewing, Routledge, ku. 117–141, ISBN 978-1-003-22349-8, iliwekwa mnamo 2025-08-26
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Duffer Brothers kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |