Dragoni-matope

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dragoni-matope

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
(bila tabaka): Bilateria
(bila tabaka): Prostomia
Faila ya juu: Ecdysozoa
Faila: Kinorhyncha
Reinhard, 1881
Ngazi za chini

Ngeli 2, oda 3

Dragoni-matope (kutoka kwa kiing. mud dragon) ni wanyama wadogo wa bahari wa faila Kinorhyncha walioenea sana kwenye matope na mchanga kwa vina vyote miongoni mwa wanyama wadogo wa sakafu. Spishi za kisasa ni mm 1 au chini, lakini zamani za kale walikuwa hadi sm 4[1].

Kiolezo cha Echinoderes akionyesha jinsi ya kusogea na kurudisha kichwa ndani.

Dragoni-matope ni wanyama wenye pingili wasio na miguu na huwa mwili unaojumuisha kichwa, shingo na kiwiliwili cha pingili kumi na moja. Tofauti na invertebrata sawa hawana silio ya nje, lakini badala yao wana idadi ya miiba kando ya mwili pamoja na duara hadi saba za miiba kuzunguka kichwa[2]. Miiba hii hutumika kwa kusogea wakisukuma kichwa mbele na kisha kushika uso wa chini kwa miiba na kuvuta mwili.

Dragoni-matope hula diatoma au dutu ya kioganiki zinazopatikana kwenye matope kulingana na spishi. Mdomo uko katika muundo wa koni kwenye ncha ya kichwa na hujifungua kwenye koromeo na kisha umio, yote mbili zilizofunikwa kwa kutikulo. Jozi mbili za tezi za mate na jozi moja au zaidi ya "tezi za kongosho" huunganisha kwenye umio na zinaonekana kutoa vimeng'enya vya kumeng'enya chakula. Mbele ya umio kuna aina ya tumbo pana linalochanganya kazi za tumbo na utumbo na kunyonya virutubisho. Utumbo mfupi wa nyuma umefunikwa na kutikulo na kumwaga kupitia mkundu kwenye ncha ya nyuma ya kiwiliwili.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 'Mindblowing' haul of fossils over 500m years old unearthed in China | Science | The Guardian
  2. Brusca, Richard C; Brusca, Gary J (2003). Invertebrates. ISBN 978-0-87893-097-5.  page 347
  3. Barnes, Robert D. (1982). Invertebrate Zoology. Philadelphia, PA: Holt-Saunders International. ku. 286–288. ISBN 978-0-03-056747-6.