Dragon Ball Super

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
dragon ball super

Dragon Ball Super (kwa Kijapani: ドラゴンボール超, Hepburn: Doragon Bōru Sūpā) ni mfululizo wa filamu ya Kijapani, muendelezo wa mfululizo wa Dragon ball z ulioandikwa na Akira Toriyama na umehadithiwa na Toyotarou na kurudiwa katika jarida la Shueisha shōnen mnamo Juni 2015.

Huo ni mfululizo wa filamu unaohusisha urafiki na burudani. Pamoja na yote haya ina ruhusa ya kutazamwa na familia yote. Katika mfululizo huu wa filamu huonyesha ujasiri na nguvu ya haki na ukweli na hata kujitolea kwa ajili ya wote uwapendao na unaowajali zaidi, ambapo nyota wa filamu hii Goku pamoja na familia yake wanashirikiana na marafiki zao ili kuhakikisha haki inatendeka.

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Katika filamu hii kuna kupitia kwa hali ngumu ambapo mkuu wa uharibifu aendaye kwa jina la Beerus aamua kuja duniani kutafuta mtu aliye na nguvu iitwayo "super seiyan god" ili kupigana naye huku duniani ndipo alipokutana na nyota wa filamu hii aitwae Goku na kumfundisha mbinu za kutumia ili aweze kufikia hatua hiyo ya super seiyan god na madhumuni makuu ya Beerus ni kumfundisha Goku ili baadaye wapigane pamoja ili kumpa Beerus changamoto katika upiganaji.baada ya mipango ya beerus kutimia na kupata nafasi ya kuwa mwalimu wa goku alimfunza yote lakini mwishoni Goku alionyesha dhahiri kuwa hana uwezo wa kufika nguvu kama super saiyan god maana nguvu hiyo inahitaji miungu na Goku akiwa mwenyewe hawezi kufikia nguvu kama hiyo.Hata baada ya yote yaliyotokea Beerus hakukata tamaa juu ya Goku na ndipo alipo pata wazo kuwa Goku akiwa mwenyewe hawezi kufikia hiyo nguvu lakini watu wenye damu ya Seiyan hata watano labda wanaweza kuunga nguvu zao zote ndani ya goku na kwa umoja wa nguvu zao wanaweza wakafikia hatua ya super seiyan god. Alijaribu kufanya hivyo kwa kuunganisha nguvu za Vegeta, Trunks,Gohan,mwana wa Gohan aliye katika tumbo la mama yake(Pan)pamoja na Goku mwenyewe na alifanikiwa kumfanya Goku kufika katika hatua hiyo ya nguvu.

Baada ya Goku kuvumbua hatua hiyo ya nguvu ya super seiyan god ndipo ulipo tangazwa mpigano huo baina ya Goku na Beerus .Mpambano huo uliitwa battle of gods"mpigano wa miungu" uliofanyika nje ya dunia katika mpigano huo Goku alipigwa pigo lenye nguvu sana lililo msababisha azimie na kudondoka kutoka nje ya dunia hadi katika bahari lakini katika moyo wa Goku kulikuwa na kumbukumbu baada ya kufikiria maneno aliyosema beerus alisema

Goku baada ya kupata mafunzo kutoka kwangu usiniaibishe utakapo pigana na mimi lasi hivyo nitailipua dunia"na kwa saabu ya maneno hayo alipandwa na hasira na kuamka juu ya maji na kwenda nje ya dunia ili apate kuendeleza mpigano baina yake yeye na Beerus. Goku alipo rudi kwa mara ya pili aljaribu kupigana na Beerus kwa nguvu zake zote kitu kilichomfanya Beerus kuzimia na kuhairisha mipango yake ya kuilipua dunia.Goku alipo muuliza msaidizi wa Beerusaitwae Whis juu ya sababu za kuzimia kwa Beerus aliwambia Beerus amekuwa akitumia mda wake mwingi kwa vitu vidogo na kutokufanya mazoezi kwa muda mrefu na alipo kuja kuuupigana na Goku kwa nguvu zake zote alizimia na kuhairisha mpango wake wa kuilipua dunia na kama Beerus atakuwa vizuri tena kiafya atarudi kuendeleza mpambano wake.

Video-x-generic.svg Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dragon Ball Super kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.