Nenda kwa yaliyomo

Dr Netumbo Nandi-Ndaitwah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Netumbo Nandi-Ndaitwah

Dr Netumbo Nandi-Ndaitwah mwaka 2025

Raisi wa Tano wa Namibia
Waziri Mkuu Elijah Ngurare
Makamu wa Rais Lucia Witbooi
mtangulizi Nangolo Mbumba

Makamu wa Raisi wa Tatu wa Namibia
Rais Nangolo Mbumba
mtangulizi Nangolo Mbumba
aliyemfuata Lucia Witbooi

Naibu Waziri Mkuu wa Namibia
Waziri Mkuu Saara Kuugongelwa
mtangulizi Marco Hausiku
aliyemfuata John Mutorwa

Waziri wa Mahusiano na Ushirikiano wa Kimataifa
Waziri Mkuu
mtangulizi Utoni Nujoma
aliyemfuata Peya Mushelenga

Waziri wa Mazingira na Utalii
Waziri Mkuu Nahas Angula
mtangulizi Willem Konjore
aliyemfuata Uahekua Herunga

Waziri wa Habari na Utangazaji
Waziri Mkuu Nahas Angula
mtangulizi Nangolo Mbumba
aliyemfuata Joel Kaapanda

Waziri wa Mambo ya Wanawake na Ustawi wa Watoto
Waziri Mkuu Hage Geingob
mtangulizi Position established
aliyemfuata Marlene Mungunda

tarehe ya kuzaliwa 29 Oktoba 1952 (1952-10-29) (umri 73)
Onamutai, South West Africa (now Namibia)
chama SWAPO
ndoa Epaphras Denga Ndaitwah

Ndemupelila Netumbo Nandi-Ndaitwah (jina la utani NNN; alizaliwa 29 Oktoba 1952) ni mwanasiasa wa Namibia ambaye amekuwa rais wa tano na wa sasa wa Namibia tangu tarehe 21 Machi 2025.[1] Pia ndiye rais wa kwanza mwanamke nchini humo. [2] Hapo awali, alihudumu kama makamu wa tatu wa rais chini ya Rais Nangolo Mbumba kati ya mwaka 2024 na 2025. Alishikilia nafasi mbalimbali za kisiasa na za uwaziri wa ngazi ya juu pamoja na majukumu mbalimbali ndani ya chama cha SWAPO na serikali yake kwa kipindi kisichokatizwa cha miaka 57.[3]

Alikuwa mgombea wa kwanza mwanamke wa urais wa SWAPO (Shirika la Watu la Kusini Magharibi mwa Afrika) mwaka wa 2024 . Mnamo 2017, Nandi-Ndaitwah alichaguliwa kuwa makamu wa rais wa SWAPO, mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi hiyo. Kabla ya kuingia katika nafasi ya juu ya uongozi, Nandi-Ndaitwah alihudumu kama naibu waziri mkuu wa Namibia kuanzia 2015 hadi 2024, waziri wa Mahusiano na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia Desemba 2012 hadi 2015, na kama waziri wa Mazingira na Utalii kuanzia Machi 2010 hadi Desemba 2012. Pia ni mbunge wa muda mrefu wa Bunge la Kitaifa la nchi hiyo.

Maisha na Elimu

[hariri | hariri chanzo]

Netumbo Nandi alizaliwa Oktoba 29 Mwaka 1952, wazazi wake walikuwa ni Justina Nekoto Shaduka-Nandi na Petrus Nandi, alizaliwa katika mji wa Onamutai, Kusini Magharibi mwa Afrika, Leo ni mpakani mwa mkoa wa Ohangwena na Oshana nchini Namibia. Baba yake alikuwa Kasisi wa Kianglikana. Alikuwa ni mtoto wa tisa kati ya Watoto 13. Ndaitwah alipata Elimu yake katika shule ya St. Mary's Mission katika eneo la Odibo.

Nandi-Ndaitwah alianza kujihusisha na siasa akiwa msichana mdogo sana, alijiunga na chama cha SWAPO akiwa na miaka 14. Akawa kiongozi wa vijana wadogo ndani ya SWAPO, Nandi-Ndaitwah alikuja kukutana na upinzani mkubwa wa kisiasa uliohatarisha maisha yake na kumbidi aishi maisha ya kujificha.

Netumbo Nandi-Ndaitwah ni mpokeaji wa tuzo za African Political Leader of the Year na African Female Leader of the Year zinazotolewa na jarida la African Leadership Magazine (ALM).[4]

Pia alitunukiwa tuzo ya Thought Leadership katika Tuzo za Maendeleo Endelevu za Namibia.[5]

Nandi-Ndaitwah pia alitambuliwa kwa Tuzo ya Uongozi wa Vizazi Tofauti (Inter-Generational Leadership Award) katika Mkutano wa Nala Feminist (Nalafem) wa mwaka 2024.[6]

Aidha, anashikilia Shahada ya Heshima ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania.[7]

  1. "Namibia will have its first female leader after the VP wins presidential election for ruling party". KTALnews.com (kwa American English). 3 Desemba 2024. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-12-09. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Namene, John-Colin (4 Desemba 2024). "Nandi-Ndaitwah elected as Namibia's first woman president". The Namibian (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 4 Desemba 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "HOME - OP - Portal Ariel". OP (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2025-08-12.
  4. "BREAKING: NETUMBO NANDI-NDAITWAH, MANDISA MAYA, OTHER LEADERS NAMED AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE PERSONS OF THE YEAR 2025 - African Leadership Magazine" (kwa Kiingereza). 2025-12-02. Iliwekwa mnamo 2025-12-03.
  5. Mukokobi, Pricilla (21 Juni 2024). "Namibia: VP Recognised for Environmental Contribution". New Era (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Septemba 2024. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2024.
  6. "VP Netumbo Nandi-Ndaitwah receives inter-generational leadership award". nbcnews.na. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Julai 2024. Iliwekwa mnamo 23 Novemba 2024.
  7. "Nandi-Ndaitwah awarded honorary doctorate by University of Dar es Salaam". nbcnews.na. Iliwekwa mnamo 23 Novemba 2024.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dr Netumbo Nandi-Ndaitwah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.