Downhill Domination

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Downhill domination ni mchezo wa kompyuta wa mashindano ya baiskeli uliotolewa na kusambazwa na PlayStation 2. mchezo huo unachezeka kutoka juu ya mlima na kushuka chini huku wakishindana na kupigana.

Mchezo huo unajumuisha mitindo tofauti ya kucheza ambao unatofautiana na michezo ya kawaida ya baiskeli.

Jinsi ya kucheza[hariri | hariri chanzo]

Kuna machaguo matatu yanayopatikana kwenye orodha kuu, ambayo ni single player,multiplayer na orodha ya chaguzi ambayo inaruhusu wachezaji kurekebisha vipengele vya mchezo kama vile kuchagua baiskeli,muendeshaji na nyinginezo.

Mbali na mashindano mengine, wachezaji wanaweza pia kufungua baiskeli na waendeshaji wenye nguvu zaidi kama Eric Carter na Tara Llanes, wakati mashindano maalum yamekwishatimia.

Kupambana pia kumeingizwa katika mchezo, ambapo mchezaji anaweza kutumia virungo viwili kushambulia washindani wengine.


Sports icon.png Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Downhill Domination kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.