Dorotheo wa Gaza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Dorotheo wa Gaza.

Dorotheo wa Gaza (Antiokia wa Syria, leo nchini Uturuki, 505 - Gaza, Palestina, 565) alikuwa mmonaki na mwandishi wa Kikristo.

Baada ya kusoma sana, mwaka 525 hivi aliamua kutawa.

Kisha kupata malezi kutoka kwa Yohane Nabii na Barsanufi wa Gaza, alianzisha monasteri mpya alipoishi hadi kifo chake, kati ya miaka 560 na 580.

Kati ya wanafunzi wake, maarufu zaidi ni Dositeo wa Gaza.

Aliacha maandishi mengi ya kiroho yanayoendelea kuzingatiwa sana hasa katika Ukristo wa Mashariki.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Juni.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.