Nenda kwa yaliyomo

Donasyani, Presidi na wenzao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Donasyani)

Donasyani, Presidi na wenzao Mansueti, Jermano na Foskolo walikuwa maaskofu wa Kanisa Katoliki katika Afrika Kaskazini ambao kwa kutetea imani sahihi waliteswa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario. Hatimaye walipelekwa uhamishoni[1].

Habari zao zimeandikwa na askofu Vikta wa Vita.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 6 Septemba pamoja na Leto wa Nefta, askofu katika Tunisia ya leo, mtu shujaa na mwenye elimu kubwa, ambaye baada ya kufungwa muda mrefu katika hali ya kutisha alichomwa moto ili kuwatisha wenzake hao [2][3].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 310-311
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 265
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.