Domosharubu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Domosharubu
Domosharubu kichwa-kijivu
Domosharubu kichwa-kijivu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Pycnonotidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
Jenasi: Bleda
Bonaparte, 1857
Ngazi za chini

Spishi 4:

Domosharubu ni ndege wadogo wa jenasi Bleda katika familia Pycnonotidae. Wanafanana na korogoto na wana rangi ya kahawa au zaituni juu na njano chini. Wanaitwa domosharubu kwa sababu wana nywele ndefu msingini kwa domo. Ndege hawa wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika kusini kwa Sahara. Tofauti na spishi nyingine za familia hii domosharubu hula wadudu hasa. Wanafuata mara nyingi makundi ya siafu na kukamata wadudu wanaotoroka. Tago lao hujengwa mtini na jike huyataga mayai mawili.

Spishi[hariri | hariri chanzo]