Dominique Voynet
Mandhari
Dominique Voynet (amezaliwa 4 Novemba 1958) ni mwanasiasa kutoka Ufaransa na mwanachama wa chama cha Europe Écologie–The Greens. Aliwahi kuwa meya wa Montreuil na pia alikuwa seneta wa Ufaransa kwa mkoa wa Seine-Saint-Denis.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Voynet alisomea udaktari na akafunzwa kuwa daktari bingwa wa usingizi (anesthetist). Wakati wa masomo yake mwishoni mwa miaka ya 1970, alianza kushiriki katika harakati za ulinzi wa mazingira (environmental activism). Alipigania dhidi ya ujenzi wa mitambo ya nyuklia katika maeneo ya Fessenheim na Malville, pamoja na ukataji miti katika eneo la Vosges kupitia Chama cha Belfort cha Kulinda Mazingira.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dominique Voynet kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |