Dolapo Oni
Dolapo Oni muda mwingine anajulikana kama Marcy Dolapo Oni ni mwigizaji, mtangazaji wa televisheni, mshauri na mshereheshaji kutoka nchini Nigeria.
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Oni ni mtoto wa mwisho kati ya watoto wanne katika familia yake. Aliishi nchini Uingereza kwa miaka 20 kabla ya kurejea Nigeria mwaka 2010.[1]
Alipokuwa na umri wa miaka 10, alitamani kuwa muigizaji baada ya kutazama tamthilia ya muziki ya Andrew Lloyd Webber iitwayo Aspects of Love katika jumba la michezo la The Oxford Playhouse.
Alipata elimu ya sekondari katika Shule ya Headington, shule ya kulipia ya wasichana mjini Oxford, Uingereza, ambako alikua msichana mweusi wa kwanza kushika nafasi ya kiongozi wa wanafunzi. Baadaye alihudhuria Chuo Kikuu cha Bristol ambako alipata shahada ya kemia.[2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Oni alianza uigizaji alipokuwa akiishi nchini Uingereza, baada ya kumaliza masomo yake ya chuo kikuu, kwa kujiunga na shule ya maigizo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "COVER STORY – DOLAPO ONI". Lady Boss. 27 Mei 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Why I left Moments with Mo – Dolapo Oni-Sijuwade". Punch. 3 Aprili 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 27 Mei 2020.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dolapo Oni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |