Djalma Santos
| Djalma Santos | |
| Amezaliwa | 27 Februari 1929 São Paulo, Brazil |
|---|---|
| Urefu | 1.73 m |
Djalma Pereira Dias dos Santos (alijulikana zaidi kama Djalma Santos; 27 Februari 1929 – 23 Julai 2013), alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Brazil aliyechezea timu ya taifa ya Brazil katika makombe manne ya dunia na kushinda mashindano ya mwaka 1958 na 1962. Santos anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki wa kulia bora wa muda wote. Ingawa alijulikana zaidi kwa uwezo wake wa kuzuia, mara nyingi alisogea mbele na kuonyesha ufundi mkubwa wa kushambulia.[1]
Pamoja na Franz Beckenbauer na Philipp Lahm, yeye ni mmoja wa wachezaji watatu pekee waliojumuishwa kwenye kikosi cha nyota wa mashindano cha kombe la dunia la FIFA mara tatu (mwaka 1954, 1958, na 1962). Hakuwa na uhusiano wa kifamilia na mshirika wake wa mara kwa mara katika safu ya ulinzi, Nílton Santos. Mnamo Machi 2004, aliteuliwa na Pelé kama mmoja wa wachezaji bora zaidi 125 waliokuwa hai. Pia ni mmoja wa wachezaji wachache wa mpira wa miguu waliocheza mechi rasmi za kulipwa zaidi ya 1,000 katika taaluma zao.[2]
Djalma Santos aliweka historia katika klabu tatu kubwa alizozichezea. Djalma alikuwa nguzo na kipenzi cha mashabiki katika klabu ya Palmeiras ya nchini Brazil, ambapo alicheza mechi 498 kwa miaka tisa na kushinda mataji kadhaa, katika klabu ya Portuguesa ya huko huko nchini Brazil, ambapo alianzia soka la kulipwa na kucheza mechi 510, na katika klabu ya Atlético Paranaense pia ya nchini Brazil, ambapo alihitimisha taaluma yake. Akiwa anajulikana kama mchezaji wa mfano wa nidhamu, hajawahi kuoneshwa kadi nyekundu wala kuondolewa uwanjani kwa nidhamu mbovu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Melinda C. Shepherd. "Djalma Santos". Encyclopædia Britannica. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2017.
{{cite encyclopedia}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Djalma Santos: Footballer who won the World Cup with Brazil". The Independent. 23 Agosti 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Agosti 2013. Iliwekwa mnamo 23 Oktoba 2013.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Djalma Santos kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |