Mwanadiplomasia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Diplomat)

Mwanadiplomasia (kutoka Kigiriki διπλωμάτης diplōmátēs, yaani mwenye hati rasmi ya kitambulisho) ni mtu aliyeteuliwa rasmi na serikali kuiwakilisha katika nchi nyingine. Taasisi za kimataifa zinazotambuliwa kama vile Umoja wa Mataifa huwa pia na wanadiplomasia.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kazi kuu za mwanadiplomasia ni uwakilishi wa masilahi ya nchi yake pamoja na raia wa nchi inayotuma. Mwanadiplomasia anatekeleza kazi katika jengo la ubalozi wa nchi yake au kama mjumbe wa utume wa kidiplomasia, mara nyingi pia katika Wizara ya Mambo ya Nje kwake nyumbani. Akiwa na cheo cha kuongoza ubalozi.

Haja ya kutambuliwa rasmi[hariri | hariri chanzo]

Mkataba wa Vienna juu ya Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961 unaeleza utaratibu unaokubaliwa na nchi zote za Dunia. Mwanadiplomasia anahitaji kibali cha nchi anakotumwa. Nchi anapotumwa inaweza kufuta kibali chake siku yoyote kwa kumtangaza ni "persona non grata", yaani kwamba hatakiwi tena. [1].

Kinga cha kidiplomasia[hariri | hariri chanzo]

Ndani ya nchi anakotumwa ana kinga cha kidiplomasia; maana yake hawezi kukamatwa kwa mashitaka, makosa au hata jinai. Anasamehewa kodi na ushuru wote kwa mahitaji yake ya kikazi na ya binafsi.

Sehemu ya kinga hiyo ni hali ya jengo la ubalozi pamoja na nyumba anamoishi balozi kuhesabiwa kuwa "nje ya nchi" (extraterritorial); mtu yeyote pamoja na maafisa wa polisi hawaruhusiwi kuingia bila kibali cha balozi mwenyewe. Kwa hiyo majengo ya kibalozi yalitumiwa wakati mwingine kuhifadhi wakimbizi waliotafutwa na serikali ya nchi yao.

Vyeo[hariri | hariri chanzo]

Mwanadiplomasia kiongozi katika nchi fulani kwa kawaida anaitwa "balozi". Akikaimu tu ataitwa "charge d'affaires". Kwa Kiingereza kuna tofauti kati ya "ambassador" na "high commisioner" ambayo ni cheo cha mabalozi kati ya nchi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "United Nations Treaty Collection". treaties.un.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-11-12. 

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • Nyeusi, Jeremy. Historia ya Diplomasia (U. ya Chicago Press, 2010) 
  • Berridge, Diplomasia ya GR: Nadharia na Mazoezi, toleo la 3, Palgrave, Basingstoke, 2005, 
  • Cunningham, George. Safari ya Kuwa Mwanadiplomasia: Na Mwongozo wa Kazi katika Maswala ya Ulimwengu Vitabu vya Maono ya Duniani 2005, 
  • Dorman, Shawn, mh. Ndani ya Ubalozi wa Merika: Jinsi Huduma ya Mambo ya nje inavyofanya kazi kwa Amerika na Chama cha Huduma za Kigeni za Amerika, toleo la pili Februari 2003, 
  • Callieres, Francois De. Mazoezi ya Diplomasia (1919).
  • Anderson, Matthew S. Kupanda kwa Diplomasia ya Kisasa, 1450-1919 (1993).
  • Nicolson, Sir Harold George. Mageuzi ya Njia ya Kidiplomasia (1977)
  • Rana, Kishan S. na Jovan Kurbalija, eds. Wizara za Kigeni: Kusimamia Mitandao ya Kidiplomasia na Kuongeza Thamani ya DiploFoundation, 2007, 
  • Rana, Kishan S. Balozi wa Karne ya 21: Mamlaka ya Udhamini kwa Mtendaji Mkuu DiploFoundation, 2004, 
  • Ernest Satow . Mwongozo wa Mazoezi ya Kidiplomasia na Longmans, Green & Co London na New York, 1917. Kitabu cha kawaida cha rejea kinachotumiwa katika balozi nyingi ulimwenguni (ingawa sio za Uingereza) Sasa katika toleo lake la tano (1998) 
  • Stevenson, David. "Wanadiplomasia" katika Jay Winter, ed. Historia ya Cambridge ya Vita vya Kwanza vya Ulimwengu: Juzuu ya II: Jimbo (2014) juzuu ya 2 sura ya 3, uk.
  • Fredrik Wesslau, Kitabu cha Washauri wa Kisiasa (2013), 
  • Wicquefort, Abraham de. Balozi na Kazi zake (2010)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]