Dionisi Ssebuggwawo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dionisi Ssebugwawo (1870 - Munyonyo, 25 Mei 1886) alikuwa mvulana wa Uganda ambaye, akiwa na umri wa miaka 16, alikiri mbele ya mfalme Mwanga, aliyekuwa anamchunguza, kwamba amewafundisha misingi ya imani ya Kikristo wenzake wawili wa ikulu, na kwa ajili hiyo alichomwa naye kwa mkuki.

Ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.

Wafiadini hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya Kabaka Mwanga II (1884 - 1903) wa Buganda ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na Kardinali Charles Lavigerie.

Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 25 Mei[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.